Thursday, April 26, 2012

Hii ni ofisi ya CHADEMA IGUGUNO, ni mji wenye idadi kubwa ya wapiga kura jimbo la iramba mashariki. Iguguno inakadiriwa kuwa na wakazi 8,000.
Mkoa wa Singida ulikuwa ni miongoni mwa ngome za CCM, alipoanza kugombea Tundu Lissu jimbo la Singida Mashariki ilichukuliwa kama anafanya mzaha mwisho wa uchaguzi aliibuka mshindi huku viti vyote vya udiwa vikitwaliwa na wana-CHADEMA.

 Hali ya kisiasa kwa Iramba Mashariki si shwari kwa CCM, Mbunge amepoteza mvuto kwa wapiga wake. Kitendo cha kuwa na madereva tisa kwa miaka miwili imeonesha ni mtu mchoyo na asiye na upendo, amekuwa mkali akifuatwa na wapiga kura wake ili awatatulie matatizo kama kiongozi wao. Badala yake amejikita kuwakatia vibarua kwenye mashamba yake ya vitunguu. 
Waliopiga kura wamekuwa wakichekwa na kukejeliwa na waliokosa bahati ya kumchagua mbunge huyo. Tundu Lissu alipofanya mkutano watu walifurika haijawahi kuotokea katika medani za kisiasa Iramba mashariki.
Aidha mambo ya kamata kamata vijana kwa kuwazushia mambo ya uzushi yamesababisha vijana kuishi kama wakimbizi kwenye nchi inayojinadi kwa utajiri wa amani. Vijana walitegemea mbunge kama mzazi wao kuwatetea haswa ikizingatiwa ni mwanamke hivyo ndio mwenye uchungu zaidi lakini amewatelekeza na kuwapa mgongo.
Pasipofanyika juhudi za haraka chama kupoteza wanachama wengi zaidi kila siku, Kipimo ni mbunge aitishe mkutano aone kama vijana wataenda kumsikiliza.  
Uchaguzi wa 2015 kutakuwa na kazi ya ziada kupiga tu kampeni, itahitaji ujasiri kukinadi chama.
Kwasasa kuna madiwani wanne wa CHADEMA jimbo hilo hii ikiwa kama mtaji mkubwa kisiasa. Vijana na akina mama wamepanga kuleta mageuzi ya kushangaza viongozi wasadiki.

0 comments:

Post a Comment