Sunday, November 11, 2012

  email E-mail this to a friend email Printable version

Questions

Mwambu, Salome Daudi  [CCM]
Iramba Mashariki Constituency
Session No Question No To the Ministry of Sector Date Asked
2 58 WORKS Transport/Road 14 February 2011
Principal Question No
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alipokuwa kwenye Kampeni za uchaguzi, aliahidi ujenzi wa daraja la Sibiti ambalo linaunganisha Wilaya ya Iramba na Shinyanga mapema iwezekanavyo.

Je, Serikali imefikia hatua gani ya utekelezaji wa ahadi hiyo ya Rais?
ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #58 SESSION # 2
Answer From Hon. Mwakyembe, Dr. Harrison George
WORKS
NAIBU WAZIRI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Salome Daudi Mwambu, Mbunge wa Iramba Mashariki, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa ahadi ya Mheshimiwa Rais ya kujenga daraja la Sibiti linalounganisha Wilaya ya Iramba na Mkoa wa Shinyanga umeshaanza. Serikali katika Bajeti ya mwaka huu wa fedha 2010/2011, imetenga jumla ya shilingi bilioni 1.304 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa daraja hili.

Tayari usanifu na uandaaji wa nyaraka za Zabuni kwa ajili ya ujenzi umekamilika. Zabuni za ujenzi wa daraja zitatangazwa katika mwaka wa fedha wa 2010/2011. Ni matarajio ya Wizara kuwa Mkandarasi atapatikana na kuanza kazi kabla ya mwisho wa mwaka huu wa fedha 2010/2011.

0 comments:

Post a Comment