Questions
|
||||||
Session No | Question No | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
---|---|---|---|---|---|---|
8 | 174 | REGIONAL ADMINISTRATION AND LOCAL GOVERNMENT | Local Government | 11 July 2012 | ||
Principal Question No | ||||||
Walimu hucheleweshwa sana kupandishwa
madaraja na pia pale wanapohamishwa hawalipwi posho za uhamisho ambazo wanatakiwa walipwe na hivyo kuwavunja moyo na kusababisha matizo ya migomo na kadhalika:- (a) Je, Serikali itamaliza lini matatizo ya walimu ili nao waishi kama wafanyakazi wengine wa Serikali? (b) Je, Serikali itachukua hatua gani kwa Wakurugenzi Watendaji wanaochelewa kuwasilisha “Seniority list” ambayo hutumika kupandishia vyeo watumishi? |
||||||
ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #174 SESSION # 8 | ||||||
|
||||||
NAIBU WAZIRI, alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Salome Daudi Mwambu, Mbunge wa Iramba Mashariki, lenye vipengele (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa walimu na kuthamini mchango wao mkubwa katika kutoa elimu nchini. Kwa kutambua hilo, Serikali imekuwa ikiboresha huduma kwa watumishi wote nchini wakiwemo walimu na kuchukua hatua mbalimbali kumaliza matatizo ya walimu ikiwemo; kuboresha viwango vya mishahara, posho nyingine ambazo watumishi au mtumishi anastahili kwa mujibu wa Kanuni. Sheria na Taratibu zilizopo, kutenga fedha za malipo ya stahili mbalimbali ikiwemo uhamisho katika Bajeti za kila mwaka na kutoa maelekezo kwa Wakurugenzi wote wa Halmashauri kuhakikisha kwamba uhamisho unafanyika pale tu ambapo fedha zimetengwa kwa ajili hiyo. Katika mwaka wa fedha 2011/2012, Serikali ilitenga jumla ya shilingi bilioni 15.8 kwa ajili ya uhamisho kwa walimu wa Shule za Msingi na Halmashauri ya Wilaya ya Iramba ilipata jumla ya shilingi milioni 131.5. (b) Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakurugenzi Watendaji kwa mujibu wa ratiba kila robo mwaka wanatakiwa kuwasilisha orodha ya ukubwa kazini (Seniority list) kwenye Mamlaka za Wizara na Tume ya Utumishi. Halmashauri zimeendelea kuandaa na kuhuisha kwa wakati orodha ya ukubwa kazini ili kuwa na taarifa sahihi za watumishi. Aidha, Serikali inaendelea kuwasisitiza Wakurugenzi kutekeleza majukumu yao ipasavyo na kuhakikisha kwamba taarifa zinazohitajika zinaendelea kuwasilishwa katika Mamlaka husika kwa wakati husika. Mheshimiwa Mwenyekiti, hivi karibuni Serikali kupitia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma (ORMUU), imeanzisha matumizi ya mfumo shirikishi wa taarifa za kiutumishi na mishahara (Human Capital Management System) ambao utapunguza kwa kiasi kikubwa tatizo la ucheleweshaji wa taarifa za watumishi kuhusiana na upandishwaji wa madaraja. |
0 comments:
Post a Comment