Questions
|
||||||
Session No | Question No | To the Ministry of | Sector | Date Asked | ||
---|---|---|---|---|---|---|
8 | 222 | FINANCE AND ECONOMIC AFFAIRS | Pension | 18 July 2012 | ||
Principal Question No | ||||||
Kuanzia mwaka 2005 Wastaafu wanalipwa kwa
mkupuo wa miezi sita sita na pensheni yao ya miaka mitatu na kwamba hulazimika kufuata mlolongo mrefu wa kujaza fomu na kuzifuatilia Dar es Salaam. (a) Kwanini Serikali imeweka tofauti katika kulipa mafao? (b) Je, ni lini Serikali itaondoa mlolongo mrefu wa kusogeza shughuli hizo mikoani? (c) Je, ni lini Serikali itatambua kuwa kiwango wanacholipwa wastaafu kimepitwa na wakati na hivyo kufanya marekebisho? |
||||||
ANSWERS TO PRINCIPAL QUESTION #222 SESSION # 8 | ||||||
|
||||||
NAIBU WAZIRI alijibu:- Kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Fedha napenda kujibu swali la Mheshimiwa Salome D. Mwambu, Mbunge wa Iramba Mashariki, lenye sehemu (a), (b) na ( c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, Serikali inawalipa wastaafu pensheni zao kupitia akaunti binafsi za wastaafu hao kwa vipindi vya miezi mitatu mitatau kuanzia Januari mwaka 2012 kama Mifuko ya Hifadhi ya Jamii inavyolipa. Asilimia 20 ya mchango wa mwanachama inatumiwa na mifuko yote. Hakuna tofauti ya muda uliopo katika kuwalipa pensheni wastaafu isipokuwa kuna tofauti ya vigezo (package factors) vya kukokotoa mafao kati ya Serikali na Mifuko mingine kama NSSF na PPF. Aidha, Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (Social Security Regulatory Authority (SSRA) kwa kushirikiana na Benki Kuu imefanya tathmini ya kuangalia namna ambavyo kila mfuko utatumia kikokotoa linganishi na mfuko mwingine katika kutoa mafao kwa Wastaafu bila kuathiri ukuaji wa mifuko. Matokeo ya tathmini hii yatawasilishwa kwa wadau wa masuala ya pensheni siku ya Ijumaa tarehe 20 Julai, 2012 kwa ajili ya kujadiliwa na kupokea mapendekezo kwa ajili ya hatua za kuandaa Waraka kwenda Baraza la Mawaziri kwa ajili ya idhini. Hivyo, ni imani ya Serikali kuwa suala la kutumia vikokotoa vipya na linganishi kwa mifuko yote ya pensheni litakamilika mapema na kuanza kutumika na wadau wote wa pensheni. (b) Mheshimiwa Spika, utaratibu wa kuzitumia Hazina Ndogo kuratibu huduma za pensheni kwa kila Mkoa na kulipa pensheni zao kupitia akaunti zao za benki unawawezesha wastaafu kupata pensheni zao huko huko walipo na hivyo sisi Serikali tunadhani utaratibu huu bado unakidhi mahitaji ya wastaafu. (c) Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kuwa kiwango cha pensheni wanacholipwa wastaafu hakikidhi mahitaji yote ya lazima. Serikali imekuwa ikiongeza kiwango cha pensheni pale ambapo uwezo wa kufanya hivyo unaruhusu. Kwa mara ya mwisho Serikali iliongeza kiwango cha chini cha pensheni kutoka shilingi 21, 601/= kwa mwezi hadi shilingi 50,114/= kwa mwezi Julai, 2009. kiwango cha shilingi 21,601/= kilianza kutumia kuanzia Julai, 2004 hadi Juni mwaka, 2009. Serikali itaangalia uwezo wake wa kumuda ongezeko la kima cha chini cha pensheni na itakapoona uwezo upo na ni endelevu haitasita kuongeza pensheni hizo. |
0 comments:
Post a Comment