Saturday, August 4, 2012

Picture
Mkazi wa jijini Dar es Saalam, Mzee James Mafita ambaye alikua mfanyakazi wa Wizara ya Kazi na Ustawi wa Jamii wa wakati huo, akitafuta wateja wa kununua boga kama alivyokutwa katika mtaa wa Mkwepu. (picha: Francis Dande/Habari Mseto blog)
WAZEE wastaafu  Serikalini wamemtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kusikiliza kilio chao cha muda mrefu ikiwemo cha kuwaongezea pensheni zao na kuwapatia kwa wakati.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, mmoja wa wazee hao James Mafita Mkazi wa Dar es Saalam, ambaye alikua mfanyakazi wa wizara ya kazi na ustawi wa jamii wakati huo, alisema kuwa zaidi ya wazee 8,000 ambao wanapata pensheni kutoka wizara ya Fedha, wamekua wakicheleweshewa kuingizwa fedha hizo licha ya kua ni kidogo.

“Mwaka, juzi, wakati wa kilele cha siku ya wazee Duniani, Oktoba Mosi, tuliweza muomba waziri mkuu atuongezee pensheni na tupate kwa wakati, lakini tunaona kimya maana kiasi cha 50,000 kwa wazee ambao hatuna kazi ni unyonyaji” alisema Mafita.

Mafita aliongeza kuwa licha  ya kuendelea kuomba ongezeko lao hilo la pensheni kwa Waziri mkuu, waliweza kuwakilisha tena kwenye kilele cha wazee mwaka jana iliyofanyika Mkoani, Lindi lakini bado hawajasilikilizwa.

“Sie wazee tumewezesha nchi hii kwa kuitumikia, lakini wameshindwa kutujali wengine tunafanya kazi kuuza maboga mitaani, lakini wao wanajipatia malupulupu umengi na kushindwa kutukumbuka” alisema Madita.

Mbali na hilo, aliomba wazira ya Fedha kuwapatia pensheni zao hizo kwa wakati kwani utaratibu uliopo sasa anawacheleweshea kwa kuwapatia zaidi ya miezi minne tofauti na awali walikua wakiwapa kwa wakati na kumtaka Pinda asikie kilio chao haraka kabla ya kuanza utaratibu mwingine kama wafanyavyo wazee wanaodai haki zao hapa nchini.

0 comments:

Post a Comment