Saturday, August 4, 2012

Muda mzuri wa kufanya hivi ni usiku.
  1. Chukua ukwaju  uliochambuliwa vizuri
  2. Loweka kwa maji ya uvuguvugu  kwa muda kidogo. Kabla ya kuloweka ukwaju hakikisha upo safi na hakuna wadudu maana ukikaa sana kuna hatari ya kuingiliwa na wadudu. 
  3. 
Baada ya ukwaju kulainika, changanya  asali, endelea kukoroga mpaka uhakikishe mchanganyiko huo umelainika kabisa.
  4. Osha uso wako kwa maji safi yenye uvuguvugu na kisha uukaushe kwa kitambaa safi, kikavu.
  5. Chukua rojo linalotokana na mchanganyiko huo kisha paka usoni
  6. Uache ukauke usoni taratibu kwa muda wa dakika kama 20.

  7. Safisha uso wako kwa maji safi, kitambaa safi na sabuni, na ukaushe na kupaka vipodozi vinavyokubaliana na ngozi yako.

Fanya hivi mara kwa mara na baada ya siku kadhaa, utaona ngozi yako inabadilika.

Imeandaliwa na Elizabeth Edward (
lizzyedu@gmail.com) via Mwananchi

0 comments:

Post a Comment