Saturday, August 4, 2012

Dr. Mwakyembe ni kati ya watu wachache nchini wanaoheshika nchini lakini kwa hili amejipunguzia maksi.

Nilikusikia mwenyewe Waziri wa Usafirishaji bungeni ukisema kuanzia septemba madereva na abiria hakuna kuchimba dawa njiani. Hivi umefanya utafiti wa kutosha kuhusu hili? Sababu ulizotoa za kusitisha uchimbaji dawa sio sahihi kwa sababu hata kule kwenye vyoo mabasi yanakosimamaga kwa chakula bado watoto na watu wazima wanachanganyika wakati wa kujisaidia kitu ambacho sio maadili yetu. Hali kama hii pia inapatikana sehemu zenye mikusanyiko mingi kama kwenye viwanja vya mipira, sabasaba, n.k. tofauti inakuwa huku kuna vyoo vya wanawake na wanaume lakinini pia hakuna vyoo vya watoto na watu wazima wa jinsia tofauti.


Lakini pia lazima ujuwe kuwa kutokana na sababu za kiafya ama hali ya hewa dereva na abiria wanaweza kushikwa na haja ndogo ama kubwa wakati wowote na popote. Hali hii ikimtokea dereva anapaswa kusimama achimbe dawa vinginevyo umakini wa kuendesha chombo cha usafiri utapungua na ajali zitaongezeka. Mfano, abiria mwenye ukonjwa wa kisukari huwa anahitaji kukojoa kila mara sawa na yule aliyepatwa na mchafuko wa tumbo anavyohitaji kwenda kuharisha kila mara. Pia watoto na mama wajawazito huwa wana vibofu vinavyojaa mkojo mapema hivyo kuhitaji kujisaidia mara kwa mara.


Hivyo basi, ili amri yako ya kutochimba dawa iheshimike lazima yafuatayo yatimizwe kwanza:

1. Vyoo vya njiani vijengwe kila baada ya umbali mfupi
2. Wagonjwa, watoto na mama wajawazito wasisafiri kwenye mabasi
3.Dereva mwenye kisukari asiendeshe gari la abiria, maana akichimba dawa zake njiani na abiria watashuka kuchimba za kwao
4. Gari likiharibika njiani litasababisha abiria wachimbe dawa hapohapo, hivyo basi, vyanzo vya kuharibika magari njiani kama vile uingizwaji matairi feki nchini, rushwa za matrafiki njiani, kujaza abiria na mizigo kupita kiasi, injini za malori, n.k vishughulikiwe kwanza
5. Uboreshwaji wa huduma za chakula njiani ili kuzuia abiria wasipate michafuko ya tumbo njiani
6. Mabasi yawe na vyombo vya kujisaidia njia (urinal bottles and bed/bus pans) ama yawe na vyoo

Vinginevyo shughulikia kwanza vyanzo vya ajari barabarani na majini, fufua usafiri wa treni, ongeza ndege badala ya kurukia mambo madogomadogo yasiyofanyiwa utafiti wa kina. tatizo la wananchi sio kuchimba dawa njiani bali.......

0 comments:

Post a Comment