Mkuu
wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Singida Mohammed Likwata
akizungumza na mwandishi wa habari wa AIM MEDIA (hayupo pichani).
Mfanyabiashara
wa bodaboda akivunja sheria ya usalama barabarani ya kupakia zaidi ya
abiria moja kama alivyonaswa kwenye kituo kikuu cha mabasi mjini
Singida.(Picha zote na Ayoub Mangi).
Na mwandishi wetu
Mkuu
wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Singida Mohammed Likwata
amewaonya madereva wa boda boda kuacha mara moja tabia ya kutumia pombe
aina ya konyagi viroba, kwa madai kuwa inachangia ajali za barabarani.
Likwata
ametoa onyo hilo wakati akizungumza na AIM MEDIA juu ya utaratibu wa
kikosi cha Usalama barabarani kuendelea kutoa elimu ya sheria za usalama
barabani kwa madereva wa bodaboda mkoani Singida.
Amesema
uchunguzi uliofanywa na kikosi chake, umebaini baadhi ya madereva wa
boda boda wana tabia ya kunywa pombe kali ya viroba (konyagi) wanapokuwa
kwenye vituo vyao, wakisubiri abiria.
Amesema
ni kosa kisheria kuendesha chombo cha moto ukiwa umelewa kwa hiyo
dereva wa boda boda akikamatwa anatumia viroba wakati wa kazi,
atakamatwa na kufikishwa mahakamani.
Pombe
inaweza pia kuwasababishia wao wenyewe, abiria na watumiaji wengine
kupata madhara makubwa ikiwemo kifo na uharibifu wa mali kama ajali
itatokea.
Katika
hatua nyingine, Likwata amewataka wamiliki wa piki piki zinazofanya
biashara za kusafirisha abiria, kutoajiri madereva ambao hajapata
mafunzo ya udereva.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa usalama barabarani mkoani Singida pekee una boda boda 231.
0 comments:
Post a Comment