Mwenyekiti
wa jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Singida na mmiliki wa kiwanda cha
usindikaji wa mafuta ya alizeti Hussein Nagi akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo kwenye picha) juu ya CCM mkoa kutoa baraka kwa amri ya
mkuu wa mkoa kupiga marufuku kwa wafanyabiashara binafsi kununua alizeti
moja kwa moja kutoka kwa wakulima. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Waziri
katika ofisi ya rais wa uwekezaji na uwezeshwaji kiuchumi Dk. Mary Nagu
(wa kwanza kushoto) akijadili jambo na mkuu wa mkoa wa Singida Dk.
Parseko Kone nje ya ofisi ya CCM mkoa wa Singida. Katikati ni katibu
mwenezi wa CCM manispaa ya Singida na msaidizi wa mbunge wa jimbo la
Singida mjini Hussein Mazala. Dk. Nagu alikuwa mkoani Singida baada ya
kutumwa na Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pind kwenda kupata taarifa sahihi juu
ya amri ya kupiga marufuku wafanyabiasha binafsi kununua alizeti moja
kwa moja kutoka kwa wakulima.
Waziri
katika ofisi ya rais uwekezaji na uwezeshwaji kiuchumi Dk. Mary Nagu
akibadilishana mawazo na katibu msaidizi wa CCM bara na mbunge wa jimbo
la Manyoni Mashariki John Chiligati (katikati)na mwenyekiti wa CCM mkoa
wa Singida Joramu Allute (wa kwanza kushoto) nje ya ofisi ya CCM mkoa wa
Singida.
Mkuu
wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone akisoma tamko lilolotolewa na CCM
mkoa wa Singida kuunga mkono amri yake (Dk.Kone) ya kupiga marufuku
wafanyabiashara binafsi kununua alizeti moja kwa moja kutoka kwa
wakulima.
Na Nathaniel Limu.
Chama
cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Singida kimebariki amri halali iliyotolewa
na mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone ya kupiga marufuku
wafanyabiashara binafsi kununua alizeti moja kwa moja kutoka kwa
mkulima.
Baraka hizo zilmetolewa na chama hicho tawala kwenye kikao chake cha halmashauri kuu kilichofanyika mjini Singida.
Kwenye
tamko la chama hicho pamoja na mambo mengine, kumedai kubaini kwamba
amri hiyo halali, haikueleweka vizuri kwa wananchi na kuagiza elimu ya
kutosha kuhusu amri hiyo, itolewe ili lengo la amri hiyo liweze
kufikiwa.
Aidha
katika tamko hilo, kimesema kuwa amri hiyo haikukataza mtu au kikundi
cho chote kununua zao la alizeti, isipokuwa imeelekeza kwamba ni vyama
vya msingi vya ushirika ndivyo vitakavyonunua moja kwa moja kutoka kwa
wakulima na kisha kuwauzia wafanyabiashara binafsi.
Tamko
hilo limesomwa na mkuu wa Singida Dk.Kone, alieagiza kwamba pamoja na
vyama vya ushirika kuwepo, kuanzishwe magulio katika maeneo mbalimbali
ambayo wakulima wa alizeti watauza kwa watu mbalimbali kwa kufuata bei
elekezi.
Akifafanua
zaidi Dk.Kone amesema hivi sasa ameteua kamati ambayo itajikita katika
kuhakiki uwepo na uwajibikaji wa vyama vya msindi vya ushirika.
Wakati
huo huo CCM mkoa wa Singida, imeagiza mamlaka zinazohusika zichukue
hatua stahiki za kuanzisha bodi ya zao la alizeti mapema iwezekanavyo.
0 comments:
Post a Comment