TIMU ya Yanga leo inakabiliwa na kibarua kigumu cha kutetea
ubingwa wake wa Kombe la Kagame mbele ya Azam katika mechi ya fainali
itakayochezwa uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Azam leo
Wakati Yanga chini ya Kocha wake Tom Seintfiet ikitaka kushinda kuweka rekodi ya kulitwaa mara ya tano tangu kuanzishwa rasmi michuano hiyo 1974, Azam wanataka kubeba mara ya kwanza.
Wakati Yanga chini ya Kocha wake Tom Seintfiet ikitaka kushinda kuweka rekodi ya kulitwaa mara ya tano tangu kuanzishwa rasmi michuano hiyo 1974, Azam wanataka kubeba mara ya kwanza.
Mbali ya Yanga kutaka kutwaa taji hilo mara ya tano baada ya kufanya
hivyo mwaka 1975, 1993, 1999 na 2011, Kocha Saintfiet, pia atakuwa
akitaka kuanza vizuri kibarua chake.
Aidha, kama Yanga itafungwa itakuwa imetema taji la michuano hiyo ililolitwaa Julai 10, 2011 chini ya Kocha
Mganda, Sam Timbe.
Kikosi cha Yanga leo
Pia, kufungwa kwake itakuwa pigo kubwa kwa uongozi mpya wa klabu hiyo
ulioingia madarakani Julai 15 kupitia uchaguzi mdogo chini ya Mwenyekiti
wake Yusuf Manji.
Mazingira hayo, yanaifanya Yanga kucheza kufa na kupona kuhakikisha
wanashinda sio tu kutetea taji, pia kuanza vizuri kwa kocha na uongozi
mpya.
Azam wao chini ya Kocha wao Stewart Hall, ni kama hawana cha kupoteza
leo kwani kwa kufika hatua ya fainali, ni fahari kwao kutokana na
kushiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza.
Wakati Yanga ikishiriki michuanio hiyo tangu kuasisiwa kwake, Azam
iliyoanzishwa Juni 24, 2007, imeshiriki mara ya kwanza, hivyo hata
ikifungwa, bado itastahili pongezi kubwa.
Mbali ya kufika fainali, Azam ni timu iliyoonyesha kiwango bora
kiuchezaji tangu hatua ya makundi, robo fainali na nusu fainali
ikiing’oa timu ngumu ya AS Vita ya DR Congo.
Sababu hizo zinaifanya mechi ya leo kuwa yenye ushindani mkali zaidi
dimbani huku Azam ikitarajia kupata sapoti kubwa ya hamasa kutoka kwa
mashabiki wa Simba.
Ingawa Yanga leo inacheza na Azam, kwa upinzani wa jadi wa wapenzi wa
soka nchini, mechi ya fainali itachukua sura ya Uyanga na Usimba.
Saintifiet kwa upande wake amedokeza kuwa, amefuatilia uchezaji wa Azam katika mechi zake na kubaini kuwa, ni
timu inayocheza soka ya kiwango cha juu, lakini hana shaka na vijana wake.
“Azam si timu ya kubeza, ni timu ambayo binafsi naihofia kutokana na
kiwango chake, nitawakabili nikijua ugumu wa mechi hiyo, kocha wao
anajua nini anafanya, lolote linaweza kutokea kesho (leo),” alisema
Saintfiet anayeweza kumpanga
beki wake Juma Abdul kutokana na kupona maumivu.
Nae Kocha Msaidizi wa Azam, Kali Ongala, alisema wamejipanga vizuri
kushinda mechi ya leo kwani Yanga si timu ngeni kwao, watahakikisha
wanaendeleza rekodi ya kuwafunga.
“Tuko fiti, naamini vijana watapambana kufa na kupona kuwafunga Yanga
kuweka rekodi ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza,”
alisema Ongala aliyekuwemo kwenye kikosi cha Yanga kilichobeba taji
hilo mwaka 1999 mjini Kampala, Uganda.
Hali ya mambo ikiwa hivyo, rekodi baina ya timu hizi, zinaibeba Azam
ambayo imeshinda mara zote nne walizokutana kati ya Septemba, 2011 hadi
Machi 10, 2012.Yanga ambayo jana ilihamisha kambi kutoka Jangwani hadi hoteli ya
Double Tree, Masaki, imefungwa mara zote mbili katika Ligi Kuu ya bara
msimu uliopita; Septemba 18, 2011 (1-0) kabla ya kulimwa 3-1, Machi 10,
2012.
PICHA ZA MECHI ZA YANGA NA AZAM UWANJA WA TAIFA JULY 26 2012.
Desemba 20, 2011, Yanga ilifungwa 2-0 katika mechi ya
Hisani kuchangia fedha za kugomboa vifaa vya walemavu zilizokuwa zimekwama bandarini.
Aidha, ushindi wa Azam wa 3-0 wa Januari 7, 2012 katika mechi ya robo
fainali ya Kombe la Mapinduzi, inaifanya Yanga kuwa na rekodi mbaya,
ingawa si kigezo pekee
cha kufungwa tena leo.
Fainali hiyo itatanguliwa na mechi ya mshindi wa tatu kati ya APR ya
Rwanda waliofungwa na Yanga 1-0 katika nusu fainali dhidi ya AS Vita
iliyofungwa na Azam 2-1.
0 comments:
Post a Comment