Saturday, July 28, 2012

HATIMAYE BARAZA LA MADIWANI WA JIJI LA MWANZA WAMNG'OA MEYA MANYARERE (CHADEMA) KWENYE WADHIFA WAKE KWA KUPIGA KURA ZA KUTOKUA NA IMANI NAYE.
 
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza jana limeng'oa kwenye wadhifa wake Meya wa Jiji hilo Bw.Josephat Manyerere(CHADEMA) kutokana na madai ya wajumbe wa baraza hilo kupitia barua walioiwasilisha Mei 24 mwaka huu iliyokuwa ikimtaka Mkurugenzi wa Jiji hilo kuitisha kikao cha dharula ili kumsomea Meya mashitaka yake.

Madiwani waliojiorodhesha na kufikia theluthi mbili ya wajumbe wapatao 17 kati ya wajumbe 33 wakiwa halali wa vikao vya baraza la madiwani wa Jiji hilo ambalo ilidai ni suala la kisheria na kanuni ya 80 za kudumu za halmashauri hiyo ambayo ipo wazi na inasomeka .

“Halmashauri inaweza kumuondoa Mwenyekiti au Meya madarakani kwa azimio linaloungwa mkono na theluthi mbili ya wajumbe kutokana na sababu yoyote ya sababu hizo ni (a) Kutumia nafasi yake vibaya(b),Kushiriki vitendo vya rushwa(c),Kushindwa kazi(d),Mwenendo mbaya wa ukosefu wa adabu na(e) lemavu wa kimwili aidha kiakili kwa kiasi cha kumfanya kushindwa kutekeleza majukumu yake kama Mwenyekiti ama Meya.”ilifafanuliwa kanuni hiyo.
Mkurugenzi wa jiji la Mwanza Wilson Kabwe.
Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza Bw.Kabwe ambaye kimsingi ndiye Katibu wa kikao hicho aliwasilisha kwa wajumbe ajenda moja tu iliyokuwa mezani ya wajumbe kutokuwa na imani na Meya hivyo kanuni ya 80 ya kumuondoa madarakani waliomba itekelezwe lakini kabla ya kufanya uamuzi huo baraza hilo lilitakiwa kujibadili na kukaa kama kamati.


Baada ya kukubalika kwa hoja hiyo Mkurugenzi Bw.Kabwe aliwataka wajumbe wasiyo wa kikao hicho cha Kamati kutoka nje ya ukumbi huku viongozi waalikwa waliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Evarist Ndikilo,RAS Bi Dorothy Mwanyika na Wakuu wa wilaya za Nyamagana Bw.Baraka Konisaga na Bi.Amina Masenza  wakitakiwa kubaki kwa mujibu wa taratibu za Halmashauri.


Hatimaye baraza lilirejea kama kawaida yake baada ya kusikiliza utetezi wa Meya Bw.Manyerere ambapo katika madai kumi yaliyowasilishwa ya tuhuma zilizokuwa zinamkabili kusomewa naye kujitetea kisha ukafanyika uamuzi wa kumpigia kura za wajumbe ili kumuondoa madarakani aidha kumuacha aendelee na nafasi yake ya Umeya.

Naibu Meya wa Jiji hilo Bw.Charles Chichibela(CHADEMA) ambaye ni Diwani wa Kata ya Mahina alitangaza matokeo ya kura hizo za wajumbe kama ifuatavyo alisema kwamba idadi ya wajumbe waliohudhulia kikao hicho wapatao 28 kati ya 33 ambao ndiyo halali lakini kutokana na wengine kuwa katika majukumu mengine ya kitaifa.

Akitangaza matokeo Naibu Meya wa jiji la Mwanza Bw. Chichibela alisema kuwa madiwani waliosema kwamba Meya Bw.Manyerere Ang’oke kwenye wadhifa huo ni wajumbe 20 na waliosema aendelee kubaki ni wajumbe nane tu (8 ) hivyo kwa mujibu wa matokeo hayo Manyerere hana tena sifa za kuwa Meya wa jiji la Mwanza.
Bwana Josephat Manyerere, Meya aliyetemwa na madiwani wa jiji la Mwanza kupitia kura za kutokuwa na imani naye hapa ilikuwa awali kabisa akiendesha kikao hicho kabla ya 'kuvulishwa joho'.
Bwana Josephat Manyerere, Meya aliyetemwa na madiwani wa jiji la Mwanza kupitia kura za kutokuwa na imani naye akitoa neno la mwisho nmara baada ya 'kuvulishwa joho'.

0 comments:

Post a Comment