*Mkutano wavurugika.
*Waunda kamati ya kusimia kijiji hicho.
*Diwani afunga mkutano.
*******
Habari na Ezekiel Kamanga,Rungwe.
Wananchi
wa Kijiji cha Isyonje,Kata ya Isongole,Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya
wamemvua uongozi,mwenyekiti wa kijiji hicho Bwana Venance Daima na
halmashauri ya kijiji kizima kwa tuhuma za ubadhilifu wa mali na
kutosimamia ipasanyo rasilimali za kijiji ikiwemo mianzi ya asili na
mashamba ya kijiji.
Tuhuma
hizo zimetolewa katika mkutano maalumu wa kijiji hicho uliofanyika Juni
28 mwaka huu mbele ya Diwani wa kata hiyo mheshimiwa Laurence Nyasa
Mfwango,ambapo baada ya kupitia taarifa ya mapato na matumizi iliyosomwa
na Afisa mtendaji wa kijiji hicho Bwana Ambokile Kinjisi na kubaini
kuwa jumla ya shilingi 1,118,000 kufunjwa na mhasibu wa kijiji Bwana
Michael Mbilinyi.
Aidha
mhasibu huyo alipotakiwa kuonyeshwa pesa hizo zilipo alishindwa hali
iliyompelekea kukiri kosa hilo na kuahidi kuzilipa Juni 29 mwaka huu
baada ya kujiwekea dhamana ya shamba la miti.
Hata
hivyo wananchi hao waliutupia lawama uongozi wa kijiji kwa kutosimamia
mali ikiwa ni pamoja na uuzaji holela wa mianzi na ukodishwaji wa
mashamba bila ridhaa ya wananchio na kutoitisha mikutano ya hadhara
ikiwa ni kinyume na kanuni za Serikali ya kijiji.
Katika
hali isiyokuwa ya kawaida baada ya tuhuma hizo wananchi walimtaka
mwenyekiti huyo na halmashauri yake kujiuzuru,ambapo walikubaliana na
kijiji hicho kusimamiwa na kamati ya mpito,chini ya Afisa mtendaji wa
kijiji Bwana Kinjisi.
Kutokana
na wananchi kuchoshwa na uongozi huo baadhi yao waliondoka mkutanoni
kwa hasira na viongozi wa kijiji kuacha viti vyao na kumuacha
Diwani,ambaye alilazimika kufunga mkutano.baada ya mwenyekiti
aliyeufungua mkutano huo na wananchi wakaridhia Kamati ya watu 10
kusimamia shughuli za kimaendeleo hadi uongozi mwingine utakapochaguliwa
kwa mujibu wa kanuni za kijiji.
0 comments:
Post a Comment