Gari
la wangonjwa la AAR ambalo lilimbeba Dk. Ulimboka likiwasili Uwanja wa Ndege wa
Mwalimu Julius Nyerere.
Baadhi
ya wanaharakati na wauguzi wakiwa na mabango yaliyokuwa na ujumbe wa kulaani
kitendo cha kikatili alichofanyiwa daktari huyo.
Mwenyekiti
wa Jumuia ya Madaktari nchini, Dk. Steven Ulimboka leo mchana alifikishwa Uwanja
wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kwa ajili ya kupelekwa nchini Afrika Kusini
kwa matibabu zaidi baada ya madaktari kubaini kuwa ana mtatizo ya kitabibu
yanayomkabili likiwemo la mtikisiko wa ubongo.
Mwenyekiti
huyo alifikishwa uwanjani hapo majira ya saa 8.30 na ndege aliyosafiri nayo
iliondoka saa 10.15. Uwanjani hapo kulikuwa na wanaharakati ambao walikuwa na
mabango, kinyume cha matarajio ya wengi walizani kuwa angeteremshwa na kuingizwa
na machela Uwanjani hapo lakini gari lililombeba lilipita moja kwa moja hadi
ndani ya uwanja huo.
0 comments:
Post a Comment