Taarifa zilizotufikia muda
huu ni kwamba,Eneo la tegeta Namanga hali ni tete mara baada ya mmiliki
wa sheli za OIL COM kwenda eneo la namanga Tegeta ambapo inasemekana
yeye alinunua eneo katika moja ya nyumba za eneo lile ambalo lina makazi
ya watu..
Oil com alikwenda pale na
watu wake(wabomoji) kwaajili ya kuvunja nyumba zile ili aweze kulichukua
neneo lake,hapo ndipo vurugu zilipoanza...kuna watu wawili wanalipotiwa
kuumizwa vibaya ambao ni wale waliokuja na OIL COM kwa ajiri ya kuvunja
eneo lile.
Wakati tukio hilo
likitokea,Msafari wa Rais ulikuwa unapita ukielekea barabara ya
Bagamoyo,alipofika eneo la tageta namanga watu ambao inasemekana
walikuwa na hasira kali walivamia msafara huo na kuanza kuupiga mawe
huku wakizomea.
Askari waliokuwepo pale
walifanya juu chini kuhakikisha msafara huo haudhuriki..Hadi nakwenda
hewani muda huu Msafara wa Rasi umeshapita,na wale majeruhi walioletwa
na mmiliki wa OIL com wamkimbizwa Hospitali kutokana na Kuvuja damu kwa
wingi.hakuna kifo kilicholipotiwa kutokea hadi sasa.
0 comments:
Post a Comment