TIMU ya soka ya Tanzania, Kilimanjaro Taifa Stars, leo inaanza
kampeni ya kusaka nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia dhidi ya
Ivory Coast ‘The Elephants’, kwenye Uwanja wa Felix Houphouet Boigny,
mjini Abidjan.
Wakati Stars chini ya kocha wake Kim Poulsen ikitaka kupata matokeo mazuri ya ugenini, Ivory Coast chini ya nahodha wake Didier Drogba, inapigana kulinda heshima yake.
Licha ya Ivory Coast kutambua ubora wa kikosi chake, mashabiki wake hawana imani na kocha mpya wa timu hiyo, Sabri Lamouchi, anayeziba nafasi ya Francois Zahoui.
Tembo hao wa Afrika, wanakutana na Stars wakiwa na shauku ya kushinda, kuwafariji mashabiki wake baada ya kuukosa ubingwa wa Afrika kwa kufungwa na Zambia kwa penalti katika mechi ya fainali ya Januari 12.
Aidha kwa Drogba ni mechi yake ya kwanza katika Uwanja wa Felix Houphouet Boigny, tangu aiwezeshe Chelsea kutwaa ubingwa wa Ulaya, Mei 19.
Kwa mchango wa Drogba katika fainali ya usiku ule dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani kwenye Uwanja wa Alliance Arena, leo anatarajiwa kuwa kivutio kikubwa kwa mashabiki.
Kingine kinachowapa matumaini katika mechi ya leo, ni ushindi wa 2-1 dhidi ya Mali katika mechi ya kirafiki iliyopigwa nchini Ufaransa.
Wakati Ivory Coast wakipata ushindi, Stars leo wanashuka dimbani wakitoka kuvuna sare ya bila kufungana na Malawi katika mechi ya kirafiki jijini Dar es Salaam.
Hesabu zinaonyesha kuwa Stars iliyo nafasi ya 145 kwenye chati ya ubora wa soka duniani, haipewi nafasi kubwa ya kuwa kitisho dhidi ya Ivory Coast.
Wakati Tanzania ikikalia nafasi hiyo kimataifa na 36 kwa Afrika, Ivory Coast ni ya kwanza kwa Afrika na 15 duniani.
Hata hivyo, Kocha Poulsen amesema hicho si kigezo cha wao kufungwa kirahisi, kwani ubora wa wapinzani wao, ni changamoto kwao ya kujituma zaidi katika mechi ya leo.
Wakati Ivory Coast ikikamia kupata ushindi wa kwanza kabla ya kukutana na Morocco katika mechi ijayo kundi C, Stars inataka kupata matokeo mazuri kabla ya kuwakabili Gambia, Juni 10 kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Ingawa hesabu zinaipa Ivory Coast nafasi kubwa ya kushinda mechi ya leo, mashabiki wanne kati ya watano, wamekuwa na hofu dhidi ya uwezo wa kocha Lamouchi.
Stars inashuka dimbani bila nyota wake wanne akiwemo kiungo Nurdin Bakari, Thomas Ulimwengu, Haruna Moshi ‘Boban’ na Nassoro Masoud ‘Cholo’ kutokana na kuwa majeruhi.
Mara ya mwisho kwa timu hizi kukutana, ilikuwa ni Januari 4, 2010 katika mechi ya kirafiki ya kimataifa iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, ambako Stars ililala 1-0 kwa bao lililotupiwa kambani na Drogba.
Kikosi cha Ivory Coast chaweza kuwa hivi: Copa, Kolo, Gosso, Souleman, Tiene, Gradel, Bony, Tiote,Yaya, Drogba na Gervinho.
Stars: Kaseja, Shomari Kapombe, Amir Maftah, Aggrey Morris, Kelvin Yondan, Shabani Nditi, Mrisho Ngassa, Jonas Mkude, John Bocco, Mbwana Samatta na Mwinyi Kazimoto.
Hii ni mechi ya kwanza ya ushindani kwa Stars chini ya udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager iliyowekeza zaidi ya sh bil. 23 kwa miaka mitano.
Mechi hiyo imepangwa kuanza majira ya saa 11 jioni za Ivory Coast, sawa na saa 2 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. CHANZO TANZANIA DAIMA

0 comments:
Post a Comment