Sasa watuhumiwa kupoteza bil. 300/-
MAWAZIRI wawili wa zamani katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige na Shamsha Mwangunga, wanatuhumiwa kuliingizia taifa hasara ya sh bilioni 300, kwa kutumia madaraka yao vibaya.
Tuhuma hizo nzito zimetolewa jana na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC), Deo Filikunjombe, ambaye alidai hasara hiyo kubwa imetokana na uzembe uliofanywa na mawaziri hao wa zamani wakati wakiiongoza wizara hiyo.
Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati hiyo na watendaji wakuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (Tanapa) Filikunjombe ambaye ni mbunge wa Ludewa (CCM) alisema kuwa Mwangunga ambaye alikuwa waziri, huku Naibu wake akiwa ni Maige, waliizuia mamlaka hiyo kutoza tozo zinazotolewa katika hoteli za kitalii kwa muda wote waliokuwa madarakani.
Alisema uzembe huo umeathiri kwa kiasi kikubwa utendaji wa serikali na iwapo shughuli hiyo ingeachiwa hifadhi hiyo ya taifa kwa mwaka wangeweza kukusanya kiasi cha sh bilioni 21.
“Pamoja na kuwa taarifa yao ni nzuri lakini sisi kama kamati tumegundua uzembe uliofanywa na Mwangunga pamoja na Maige juu ya jambo hilo maana fedha hizo zingeweza kujenga barabara na shule kila maeneo,” alifafanua.
Alisema matatizo mbalimbali yanayolikabili taifa hili yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na wanasiasa hivyo aliwataka kuacha shughuli za mashirika kufanywa na bodi walizonazo.
“Matatizo mengi yanayojitokeza ni kutokana na wanasiasa kuingilia moja kwa moja shughuli zinazofanywa na mashirika kama ambavyo tumeliona hili lililowapata TANAPA ambapo kuna maamuzi ya kisiasa yaliyofanywa na Mwangunga pamoja na Maige,” alisema.
Alisema kipindi cha uwaziri wa Maige alishindwa kulipatia ufumbuzi suala hilo kwani alilichochea hatua iliyohamasisha waliokuwa wakipinga uamuzi huo kukimbilia mahakamani.
Alisema hadi sasa TANAPA imepata kiasi cha sh bilioni 4 pekee katika tozo za hotel hizo zilizo katika hifadhi mbalimbali nchini, hivyo kamati imeazimia kukutana na wizara hiyo ili kuangalia namna ya kulishughulikia tatizo hilo.
Machi 21, 2011 wizara hiyo ilitetea sakata hilo la tozo huku ikimkingia kifua aliyekuwa Waziri Ezekil Maige kuwa hausiki na jambo hilo.
Katika taarifa hiyo ambayo ilitolewa na msemaji wa Wizara hiyo George Matiko, ilieleza kuwa mtangulizi wa Maige katika wizara hiyo Shamsa Mwangunga, ndiye aliyekubaliana na pingamizi la wadau ambao hawakukubaliana na ongezeko hilo na kuliagiza shirika la hifadhi za taifa (Tanapa) kusitisha utekelezaji wa tozo mpya.
Alisema Tanapa katika mwaka wa fedha 2008/09 lilipendekeza kuongezwa kwa tozo za watalii wanaolala katika hoteli na kambi za wageni ndani ya hifadhi za taifa na kwamba ongezeko hilo lilifuatia vikao vya pamoja kati ya shirika hilo na wadau mbalimbali katika sekta husika na wengi wao walikubaliana na ongezeko hilo.
Kwa mujibu wa Matiko, wadau wachache katika sekta hiyo ya hoteli hawakuridhika na uamuzi huo wa kuongeza tozo hilo na waliamua kupeleka suala hilo wizarani wakitaka kusitishwa kwa uamuzi huo wakidai kuwa utaathiri biashara zao.
Kuibuka kwa tuhuma hizo kumezidi kuwaweka waliokuwa mawaziri wa wizara hiyo katika wakati mgumu wa kujinasua na sakata nzito zinazojitokeza kila siku.
Kamati za Bunge zacharuka
Katika vikao vyake, Kamati mbalimbali za Bunge zimecharuka na kuchukua maamuzi mazito yakiwemo ya kuwatimua watendaji wa halmashauri kadhaa baada ya kutoridhishwa na ripoti za utendaji kazi.
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) imekataa kupitia na kukagua hesabu za halmashauri za Rufiji na Mafia na kulazimika kuwatoa nje kutokana na kushindwa kuwasilisha taarifa za hesabu zao kwa wakati mbele ya kamati hiyo.
Licha ya kuwatoa nje pia wajumbe wa kamati hiyo wamewataka wakurugenzi na wakuu wa idara wa halmashauri hizo kukatwa asilimia 15 ya mishahara yao kwa mwezi Juni ikiwa ni adhabu kutokana na uzembe huo.
Mwenyekiti wa kamati hiyo, Augustino Mrema, alisema wajumbe wa LAAC wametoa wiki mbili kwa halmashauri hizo kurekebishe hesabu zao na kuziwasilisha mbele ya kamati hiyo pamoja na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Mrema ambaye ni mbunge wa jimbo la Vunjo (TLP) alisema kamati yake inadhamiria kumshauri Rais Jakaya Kikwete kuwawajibisha watendaji wazembe na wanaotuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha na mali za umma.
Alisema operesheni ya kusafisha nchi na kuwaondoa mafisadi wanaofuja fedha na mali za umma ni zoezi endelevu kwa halmashairi zote nchini.
Mwenyekiti huyo hakusita kutoa onyo kali na kutangaza vita kwa wakurugenzi wa halmashauri nchini ambao wanajihusisha na ufujaji wa fedha za umma huku wakipuuza maagizo yanayotolewa na kamati yake na kuwa hawatasita kuwawajibisha.
“Tuliamua kuwatoa nje ya mkutano na kukataa kupitia hesabu zao kutokana na kuchelewa kuwasilisha vitabu vyao mbele ya kamati...vitendo vya aina hiyo vinaonyesha kudharau maagizo ya Bunge,” alisema.
Michango ya mafuriko yaibiwa
Nayo Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC), imeagiza serikali kuwalipa fidia wananchi wa Mabwepande walioporwa viwanja na kupewa wahanga wa mafuriko.
Aidha kamati hiyo, imebaini upotevu wa vifaa vilivyotolewa kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokea mwishoni mwa mwaka jana ambao wamehamishiwa katika eneo la Mabwepande nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza jana mara baada ya kutoka kutembelea waathirika hao, Makamu Mwenyekiti wa PAC, Zainabu Vullu (CCM), alisema wajumbe wa kamati hiyo wamebaini upotevu wa mabati 40, saruji mifuko 44, nguo na magodoro.
“Kuna mifuko 1,500 ya saruji ikiwa inaanza kuharibika bila ya kutumika kwa matumizi yaliyokusudiwa hivyo tumeagiza wahusika kufanya uhakiki ‘stock checking’,” alisema.
Kutokana na hali hiyo kamati imeipa wiki mbili Ofisi ya Waziri Mkuu, Kitengo cha Maafa, itoe maelezo ya upotevu wa vitu hivyo mbele ya kamati hiyo bungeni mjini Dodoma.
Nayo Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imewabana Watendaji wa Mkoa wa Kagera kwa kuidhinisha sh bilioni 4.5 katika mradi wa ujezi wa gati katika ziwa ambao mradi huo hauendani na fedha hiyo.
Kutokana na madudu ya mkoa wa Kagera imemwita aliyekuwa Katibu Tawala Maria Bilia ambaye sasa ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kuidhinisha mradi ambao hauwezi kutekelezeka kutokana na bajeti kuwa finyu.
Wabunge wamelalamikia mradi wa bilioni 4.5 kuwa ni mkubwa ambao hadi hatua ya mwisho wametumia sh bilioni 1.5 kwa ujenzi ambao hauendani na thamani ya fedha.
Akizungumza jana Mwenyekiti wa Kamati hiyo, John Cheyo, alisema kuwa matumizi ya serikali kwa mkoa huo ni mabaya, na akataja matumizi ya fedha za ujenzi wa gati kwenda kujenga majengo ambayo hayakuwa kipaumbele.
Cheyo alisema kuwa mkoa huo umepata hati yenye mashaka katika miaka miwili mfululizo kutokana na kutumia fedha ya wanyonge katika miradi mikubwa ambayo inatumia fedha nyingi lakini haishi.

CHANZO TANZANIA DAIMA
0 comments:
Post a Comment