WAZIRI wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, ametengua nafasi ya
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL), Paul
Chizi, kwa madai kuwa uteuzi wake haukufuata sheria, kanuni na taratibu
za utumishi wa umma.
Badala yake Dk. Mwakyembe amemteua Kapteni Lusajo M Lazaro, kukaimu nafasi hizo kuanzia Juni 4.
Aidha Mwakyembe amewasimamisha kazi maofisa wengine wanne wa ATCL akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Uhandisi John Ringo.
Maofisa hao ni pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Fedha, Justus Bashara, na Kaimu Mkurugenzi wa Biashara,
Josephat Kagirwa, pamoja na Mwanasheria, Amin Mziray.
Taarifa ya Wizara ya Uchukuzi iliyosainiwa na Katibu Mkuu wake, Omary Chambo, ilisema kuwa kusimamishwa kazi kwa maofisa hao kunatokana na ukiukwaji wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma ambao umetishia uhai wa chombo hicho muhimu kwa taifa.
Kutokana na ukiukwaji huo, taarifa hiyo ilisema kuwa wizara itaunda kamati ya wajumbe watatu wenye uelewa wa mambo ya fedha na sheria ili kuchunguza matumizi ya fedha zilizotolewa na serikali kwa kampuni hiyo kuanzia mwanzoni mwa Mei mwaka huu.
“Chizi Paul aliteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ndege (ATCL) Agosti 6, 2011, hata hivyo utaratibu wa uteuzi wake haukufuata sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma,” ilisema taarifa hiyo.
Katika taarifa hiyo, Mwakyembe amefikia uamuzi huo kwa mujibu wa sheria namba 8 ya mwaka 2002 na Kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003 namba 17(4).
Hata hivyo taarifa hiyo ilieleza bayana kwamba endapo mtumishi ameteuliwa kwa kukiuka kifungu cha 17 (1) au (3) za kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003, itakuwa ni mamlaka ya uteuzi ambayo ina mamlaka ya kutengea uteuzi wake mara moja.
Hivi karibuni ATCL, imekuwa ikifanya kazi kwa kulegalega kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kutokuwa na ndege baada ya iliyokuwa ikitoa huduma kupata ajali na kuharibika mkoani Kigoma.
ATCL ilikuwa na ndege mbili ambapo moja iliharibika mkoani Mwanza na kubaki moja ambayo ilikuwa ikifanya safari sehemu mbalimbali nchini. Kwa sasa kampuni hiyo ina ndege moja ya kukodi.
CHANZO CHA HABARI: http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=36673 na na Datus Boniface

0 comments:
Post a Comment