WATU tisa wamefariki papo hapo na wengine 20 kujeruhiwa katika
ajali iliyohusisha magari mawili eneo la Ntangano Ijombe Mbeya Vijijini
barabara ya Mbeya- Kyela.
Ajali hiyo imelihusisha roli lenye namba za usajili T.658 ASJ lililokuwa na tela namba T.150 ASN iliyokuwa ikitokea mpakani mwa Tanzania na Malawi (Kasumulu) pamoja na Costa yenye namba T.886 BDZ iliyokuwa ikitokea jijini Mbeya kuelekea wilayani Kyela.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Rufaa Mbeya Dk. Eliuter Samky amethibitisha kupokea maiti tisa wakiwamo wanawake watatu pamoja na majeruhi 20 na kusema kuwa mara baada ya majeruhi kufikishwa hospitalini hapo watu wanne walipoteza maisha wakiwa katika harakati za kupatiwa matibabu.
“Ni kweli tumepokea idadi hiyo ya maiti lakini kati ya majeruhi 20 tuliowapokea tayari wanne wamepoteza maisha na wengine watatu wako katika hali mbaya na wamelazwa katika chumba cha wagonjwa wa dharura,” alisema Dk. Samky.
Aidha alisema majeruhi wengine 16 wanaendelea kupata matibabu hospitalini hapo kwa kuchukuliwa vipimo wakati watakaokuwa wamepata matibabu wataruhusiwa kwenda nyumbani.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, ilitokea majira ya saa nane kasoro robo mchana ambapo roli likiwa katika mwendo kasi likijaribu kukata kona kali lilizidiwa hivyo tela kuigonga Costa na kusababisha ajali hiyo.
Akizungumza katika eneo la tukio Safari Samson shuhuda wa ajali hiyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa dereva wa Costa aliyemtambua kwa jina moja la Mwasa mkazi wa Ilomba jijini Mbeya ni mmoja wa watu waliofariki papo hapo.
“Nimefika eneo hili mapema sana kwani Costa hii ni ya ndugu yangu baada ya kupigiwa simu kuwa gari ya ndugu yangu imepata ajili, nilishuhudia maiti nane ikiwamo ya dereva wa Costa zikitolewa eneo hili na kwenye roli tumetoa maiti moja ambapo dereva wa roli amekimbia,” alisema.
Naye utingo wa roli lililopata ajali, Christopher Mgaya (32), mkazi wa Dar es Salaam alisema kuwa walikuwa wakitokea mpakani kuelekea Dar es Salaam wakishuka katika mtelemko kwenye kona aliona Costa ikipandisha mlima ghafla tela lilicheza ndipo mwenye Costa akajibamiza kwenye tela na kusababisha ajali hiyo.
“Kwenye roli tulikuwa watatu, mimi, dereva ninayemtambua kwa jina moja tu la Peter pamoja na abiria mmoja ambaye tulimpakia akiwa na mzigo wake wa maparachichi na machungwa hata hivyo alifariki, lakini dereva amenieleza kuwa shingo inamuuma sana hivyo ametangulia hospitali.
http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=36675

0 comments:
Post a Comment