Huku ulimwengi ikiadhimisha siku
ya uhuru wa vyombo vya habari, mwandishi mmoja wa habari wa kituo cha
redio cha Daljir, nchini Somalia, ameuwawa kwa kupigwa risasi na watu
walio kuwa wamejihami kwa silaha kali mjini Galkayo Kaskazini mwa nchi.
Hilo ni tukio la tano la mauaji ya aina hiyo kufanyika mwaka huu.
Mwandishi wenzake wa habari wa kituo hicho cha
redio, Farhan Jeemis Abdulle, amesema kuwa wakati akitoka ofisini,
walifyatuliwa risasi na watu walikuwa wameficha nyuso zao.
Shirika la Uhuru wa Vyombo vya Habari la
Reporters Without Borders, limesema Somalia ni nchi hatari kuliko zote
kwa mtu kufanyakazi ya uandishi wa habari.
Zaidi ya waandishi wa habari 30 wameuawa katika kipindi cha miaka 5 iliyopita Somalia
0 comments:
Post a Comment