Thursday, May 3, 2012


Sol Campbell
Sol Campbell
Aliyekua beki wa timu ya Taifa ya England Sol Campbell ametangaza kustaafu mchezo wa soka akitamatisha kipindi cha miaka 19 ambapo aliichezea klabu ya Tottenham kabla ya kufanya uwamuzi wa kuchukiza mashabiki wa klabu hio akihamia katika klabu inayohasimiana ya Arsenal.
Campbell mwenye umri wa miaka 37 -ni mchezaji aliyetumia nguvu wakati wa uchezaji wake kama beki wa kati aliyeichezea England mara 73, ameamua kustaafu baada ya kukosa klabu ya kumkubali baada ya Newcastle kukatisha mktaba wake mwishoni mwa msimu ulipita.
Mashabiki na wapenzi wa soka watamkumbuka zaidi siyo kwa uchezaji wake bali kwa uwamuzi wake wa kuhama kutoka Tottenham na kujiunga na Arsenal mnamo mwaka 2001, akizusha chuki zaidi kutoka kwa mashabiki wa Spurs.
Wakati wake alishinda mataji mawili na Arsenal, Ligi kuu mara mbili na kombe la FA mara mbili aliposhiriki na timu ya msimu wa mwaka 2003-04 iliyoacha sifa kua Invincibles iliyopitia kipindi bila kufungwa.
Alirejea kuichezea Arsenal kwa mkopo mwaka 2010, na pia kuichezea Portsmouth na Notts Coounty.
Campbell ambaye alibahatika kushiriki kombe la Dunia mara tatu na mashindano ya Ulaya mara tatu, hakuwahi kubadili klabu kwa malipo.
Andrey Arshavin
Andrey Arshavin
Wakati huo huo Andrey Arshavin anasema kua atasubiri hadi kumalizika kwa fainali za Euro 2012 kabla ya kuamua hatma yake.
Arshavin alijiunga na klabu ya nyumbani kwao ya Zenit St Petersburg kwa mkopo wa miezi mitano mnamo mwezi Febuari ambapo ameisaidia klabu hio kushinda Ligi ya Urussi kwa mara ya pili.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 hana hakika kama atarudi kuichezea Arsenal msimu ujao au la, na ameamua kuahirisha mazungumzo juu ya hilo.

0 comments:

Post a Comment