Thursday, May 24, 2012

Jeshi la Syria linahusika na ukiukwaji wa haki kwa kiasi kikubwa na vitendo vibaya vya uvunjaji wa haki za binadamu tangu mwezi March mwaka huu, kwa mujibu wa ripoti ya Tume ya Umoja wa Mataifa.
Ripoti hiyo imetaja pia mbinu za wapinzani kukiwa na ushahidi wa kukamatwa na kuteswa na pia kuuawa kwa askari.
Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wanasema mgogoro huo unaongezeka kuwa wa kijeshi zaidi.
Kwa mujibu wa Umoja huo wa Mataifa idadi ya watu waliokufa ni zaidi ya watu 9,000 tangu ghasia hizo za kumpinga Rais Assad zianze mwez Machi 2011.
Katika ripoti ya hivi karibuni kuhusu Syria ya miezi ya Machi, April na kwa sehemu Mei, waangalizi kutoka Baraza la Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu waliteua tume huru ya uchunguzi Syria na kupata matukio ya utesaji na mauaji yaliyofanywa na pande zote mbili Jeshi la Syria na vikosi vya upinzani.

CHANZO: BBC SWAHILI>>http://www.bbc.co.uk/swahili/news_in_brief/2012/05/120524_syria_human_rights.shtml

0 comments:

Post a Comment