Vatcan
imempongeza Mshambuliaji wa Ivory Cost na CHELSEA kwa kuishuhudia imani
yake mbele ya ulimwengu mzima na kwa kudhihirisha anavyomtegemea Mungu
katika Maisha yake.
Nyota huyo
wa soka Mkatoliki alipiga ishara ya msalaba hadharani baada ya kufunga
bao la kusawazisha dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani kwenye mchezo wa
fainali wa club bingwa ya ulaya, dakika ya 88 ya mchezo. Drogba alirudia
kupiga ishara ya msalaba kama ishara ya kumshukuru Mungu katika Muda wa
ziada baada ya Mchezaji Robin kukosa penalt iliyokuwa imesababishwa na
yeye Drogba.
Kana kwamba haitoshi, Drogba alionekana amepiga
magoti akisali wakati wapinzani Munich wanapiga penalti ya mwisho ya
maamuzi, akijiandaa kwa zamu yake ya kwenda kupiga penalt ya mwisho kwa
upande wa timu yake.
Na hatimaye Drogba akapiga ishara ya
msalaba ya wazi zaidi kama kitendo cha kwanza kabisa baada ya kufunga
penalt ya ushindi iliyoipa ubingwa Chelsea, tofauti na matarajio ya
wengi kwamba angeanza kukimbia kurukiana na wenzake kabla ya kuukumbuka
mchango wa Mungu kwenye kufunga kwake penalt ile muhimu.
Kana
kwamba haitoshi, Drogba alipofuatwa na waandishi wa habari kutaka maoni
yake baada ya ushindi, swali la kwanza aliloulizwa lilikuwa "What do you
tel the world today Drogba", yaani "Unauambia nini ulimwengu leo
Drogba". Jibu la kwanza la Drogba lilikuwa: "Glory be to God. At last we
have accomplished the mission". Yaani "Utukufu kwa Mungu, hatimaye
tumetimiza ndoto".
Vatcan imesisitiza kwamba ni mara chache
sana kukuta nyota wa kiwango kikubwa ulimwenguni katika fani yoyote
anamtegemea Mungu waziwazi katika fani yake, na anamtukuza Mungu bila
kuficha mpaka kilele cha mafanikio yake.
MIMI NA WEWE TUNAJIFUNZA NINI HAPA?
0 comments:
Post a Comment