Baraza la Kitaifa la Upinzani
nchiniSyria(the SNC) limesema limekubali kujiuzulu kwa Rais wake Burhan
Ghalioun, ambaye ameongoza vuguvugu hilo tangu lianze mwezi September
mwaka jana.
Limesema Bw Ghalioun ataendelea kuliongoza Baraza hilo mpaka atakapopatikana mrithi wake.Bw Ghalioun alishachaguliwa mara tatu, na hivi karibuni mwezi huu lakini uongozi wake katika SNC umekuwa ukikosolewa na wanaharakati hasa wale walio ndani yaSyria.
Baraza hilo la SNC limekuwa likosolewa pia kwa kushindwa kupata ushawishi na kuungwa mkono na Jumuiya ya kimataifa katika harakati zake nchini Syria.
Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa idadi ya watu waliokufa ni zaidi ya watu 9,000 tangu ghasia hizo za kumpinga Rais Assad zianze mwez Machi 2011
CHANZO CHA HABARI:BBC SWAHILI
http://www.bbc.co.uk/swahili/news_in_brief/2012/05/120524_syria_opposition_resgination.shtml
0 comments:
Post a Comment