IMEDAIWA kuwa wahadhiri wengi vyuo vikuu nchini wanakabiliwa na tatizo
la kukumbwa na msongo wa mawazo kuliko wafanyakazi wengine nchini.
Uafiti
uliyofanywa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuhusu msongo wa mawazo
kwa wafanyakazi mbalimbali nchini ulibaini kwamba wafanyakazi wa vyuo
vikuu wako hatarini kukumbwa na tatizo hilo.
Akizungumza katika
mkutano wa uzinduzi wa ripoti ya utafiti huo, Mkuu wa Idara ya Elimu ya
Saikolojia na Mitalaa, Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Dk Kitila Mkumbo
alisema kuwa utafiti umevihusisha vyuo vinne.
Vyuo vilivyohusishwa ni
Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Chuo Kikuu cha Tumaini, Chuo Kikuu cha
Dodoma na Chuo cha Mtakatifu John’s na kubaini wafanyakazi wanaofanya
kazi katika vyuo hivyo wakiwa na tatizo hilo.
Dk Kitila alisema
sababu kubwa zinazosababisha Wahadhiri kuwa na msongo wa mawazo ni
kutokana na kufanya kazi kwa muda mrefu bila kupumzika na kwamba wengine
wanashindwa kutimiza malengo yao kama vile machapisho ya kutosha kwa
mwaka pamoja na matatizo ya wanafunzi.
Kutokana na hali hiyo, Dk
Kitila alishauri waajiri kuwaandalia mazingira mazuri ya kufanyia kazi
ikiwa ni pamoja na kuwaajiri wanasaikolojia katika taasisi zao ili
kuweza kuwashauri waajiri na waajiriwa.
“Unajua sababu kubwa
zinazowasababishia msongo wa mawazo wahadhiri wanafanya kazi nyingi
sana, mara nyingi wengine wanashindwa kuchapisha machapisho ya kutosha
huku matatizo ya wanafunzi nayo yanakuwa mengi kama vile kushindwa
kumaliza kazi wanazopewa,”alisema Dk Kitila.
Alisema kuwa wafanyakazi
wengine wanakumbwa na msongo wa mawazo kutokana na kukosa vitendea kazi
vya kutosha pamoja na migogoro kazini.
Alitoa wito kwa waajiri na
waajiriwa kuepuka migogoro isiyo ya lazima kazini ili kuepuka mambo
ambayo yanaweza kusababisha msongo wa mawazo hali inayosababisha
mfanyakazi kufanya kazi vizuri.
Home
»
»Unlabelled
» Wafanyakazi vyuo vikuu hatarini kwa msogo wa mawazo
Thursday, April 26, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment