Majaji katika mahakama maalum kuhusu vita nchini
Sierra Leone, leo watatoa hukumu dhidi ya aliyekuwa Rais wa Liberia
Charles Taylor kwa kuhusika na vita hivyo vilivyodumu miaka 10.
Taylor anakabiliwa na mashtaka 11 ikiwemo ubakaji na mauaji ya raia wa Sierra Leone.
Kiongozi huyo wa zamani anadaiwa kufadhili waasi wa RUF.
Zaidi ya mashaidi 100 wamefika mbele ya mahakama
hiyo lakini Bw Taylor amekanusha kuhusika na uhalifu huo wakivita na
anadai kuwa kesi hiyo ni njama ya kummaliza kisiasa.
Hukumu ya majaji hao inasubiriwa kwa hamu sana
na raia nchini Sierra Leone ambao jamaa zao waliathirika sana wakati wa
vita hivyo.
Inakadiriwa kuwa zaidi wa watu elfu 50 waliuawa
na wengine wakiwemo wanawake na watoto walibakwa na kukatwa mikono au
miguu na waasi wa RUF ambao upande wa mashtaka unasema walipata usaidizi
wa silaha kutoka kwa Bw Taylor.
Wakati wa vita hivyo, mwendesha mashtaka anasema
kuwa Taylor alikuwa kiungo muhimu katika biashara haramu ya almasi
kutoka Sierra Leone.
Kesi hii iliodumu miaka mitatu na nusu, hata
hivyo huenda isi kamilike leo kwani pande zote wanauhuru wa kukata rufaa
ikiwa hukumu hiyo
0 comments:
Post a Comment