Saturday, August 17, 2013

Picture: Dk Mwakyembe
Dkt. Mwakyembe akionyesha picha ya Agnes Gerald "Masogange" kwa wanahabari
Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa agizo kwa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) kuwafukuza kazi na kuliagiza jeshi la Polisi nchini kuwaunganisha na wengine kwenye kesi mahakamani ili kujibu mashitaka ya jinai chini ya sheria ya kuzuia dawa za kulevya, wale wote waliohusika katika kuuwasaidia Agnes Gerald na mwenziye Mellisa Edward kupitisha dawa za kulevya aina ya Crystal Methamphetamine "TIK" au "Meth" au "USAN" kilogramu 180 kuelekea Afrika Kusini Julai 5, ambako walikamatwa katika kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha O. R. Tambo nchini humo.

Waziri Mwakyembe ametoa agizo hilo leo, ofisini kwake, mbele ya waandishi wa habari wakati alipowaita ili kuufahamisha umma kuhusu hatua zilizochukuliwa na Wizaa yake kuhusu suala la dawa za kulevya.

Maafisa Usalama wa JNIA waliofukuzwa wametajwa kuwa ni:-

    Yusuph Daniel
    Jackson Manyoni
    Juliana Thadei
    Mohammed Kulangwa
    Koplo Ernest (askari polisi)

Aidha, Waziri Mwakyembe ameiagiza idara ya Usalama wa Taifa kufanya uchunguzi wa kina kwa maafisa wake waliokuwa zamu siku ya tukio kwa kuchelewa kuwafikisha mbwa kwa muda muafaka.

Dk Mwakyembe arudia kauli yake ya jana kwa kusisitiza kuwa kuanzia sasa watu wote watakaokamatwa wakisafirisha dawa za kulevya watapigwa picha ambazo zitaoneshwa wazi kwa wananchi.
Picture: Agness Gerald 'Magange'
Agnes Gerald

0 comments:

Post a Comment