Biashara ya binadamu imeibuka kwa kasi nchini na kutishia usalama wa nchi kutokana na watoto wenye umri kati ya miaka 8-15 baadhi yao w...
TMA yatoa tahadhari ya mvua kubwa kutokakana na kimbunga FELLENG
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, TMA, inauhadharisha umma kuhusu hatari ya uwezekano wa kuwepo kwa mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo nchi...
Wabunge, A. Abdallah, M. Kasembe wazungumzia kuharibiwa mali zao
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Maria Mzuki amesema Polisi inawashikilia watu 44 wilayani Masasi kwa tuhuma za kujihusisha na vurugu...
Mwanaume mpambanaji: Godoro kichwani, mwana mgongoni, begi begani
KAMERA za blogu ya Dustan Shekidele asubuhi ya Januari 15, 2013 ilimemnasa mwanaume huyu ambaye jina lake halikupatikana mara ...
Taarifa ya Habari Januari 28, 2013 28/01/2013 0 Comments Taarifa - TBC Add Comment Kikao cha Wanamtwara na Waziri Mkuu - Dondoo za yaliyojiri (audio) 28/01/2013 1 Comment Picture Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya siasa na viongozi wa Asasi mbalimbali kuhusu mgogoro wa gesi kwenye ukumbi wa VETA mjini Mtwara Januari 27, 2013 Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda yupo Mkoani Mtwara akikutana na makundi ya wadau mbalimbali wa mkoa huo ili kusikia kutoka kwao mawazo, michango na dukuduku zao kuhusu mradi wa gesi asilia. Imeripotiwa kuwa Waziri Mkuu angekutana na wanahabari baadaye leo saa 9 alasiri ili kutoa mjumuisho wa maongezi yake. Taarifa mpya zitawekwa hapa punde zitakazopatikana. Kwa sasa, tafadhali sikiliza rekodi ya kipindi cha Amka na PRIDE FM radio, kilichozungumzia muhtasari wa yaliyojiri katika kikao cha jana kati ya Waziri Mkuu na Wadau. (Pleya zipo za aina mbili ili kuongeza wigo wa uchaguzi wa urahisi wa kifaa chako kwa ajili ya kusikiliza.) Mtwara na Waziri Mkuu - PRIDE FM UPDATES/TAARIFA MPYA za ziara ya Waziri Mkuu kutoka kwa Baraka Mfunguo - MtwaraKumekucha blog Waziri Mkuu alikuwa akutane na Waandishi leo saa tisa alasiri. Kutokana na kikao kirefu cha madiwani wa Manispaa ya Mtwara/Mikindani na Mtwara vijijini pamoja na kikao cha wafanyabiashara, majumuisho ya ziara ya Mtwara atayatolea ufafanuzi kesho. Kwa sasa (jioni) anakula chakula na kikao cha Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Mtwara kitafuatia. Kutokana na kuwepo kwa makundi katika Kamati ya Siasa ya CCM-Mkoa, wabashiri wengi wanasema kikao hicho kitakuwa na mvutano mkali. Dondoo muhimu: Kwa ufupi wajumbe wengi wamekataa bomba la gesi lisiende Dar Wamemkataa Mkuu wa Mkoa na kumtaka Waziri Mkuu aondoke naye Wajumbe (Madiwani ) kumpinga kwa kauli moja Hawa Ghasia kwa kile kilichosemwa kutumia mamlaka kutoa kauli za uongo kuhusu Mtwara Vijijini kuunga mkono suala la gesi iende Dar madiwani waMtwara vijijini. Wamesema hawakushirikishwa. Mzozo wa viwanja baina ya Madiwani na Mkuu wa Wilaya Waziri Mkuu ametumia mbinu ya kisiasa kuwashawishi Wadau kuwa bomba liende Dar Wajumbe wameondoka kwa shingo upande kwa kukubali kutokubaliana na Waziri Mkuu Kikao kinafanyika chini ya ulinzi Mkali wa FFU, JWTZ na UwT (Usalama wa Taifa) Hawa Ghasia arudishwa Uwanja wa Ndege, JKNIA asije Mtwara kwani anaweza kuchafua hali ya hewa Polisi wanadai Meya anataka kuwachonganisha na jamii/wananchi kutokana na kauli yake ya kusema wao ndio chanzo cha vurugu 1 Comment Malaika Orphanage Foundation ikakukaribisha uwe mdau wa kituo 28/01/2013 0 Comments Picture Wikiendi hii Mkurugenzi na muasisi wa kituo cha kulelea watoto yatima,kinachoitwa Malaika Orphanage Foundation, Rahma Manji (pichani kushoto) alipokea msaada kutoka kwa mwambata wa jeshi kutoka nchini Ujerumani, Bw Abel Gunta (pichani kulia) ambaye aliguswa na moyo wa mwenyekiti huyo aliyemua kuanzisha kituo cha kusaidia watoto baada ya yeye mwenyewe kujikuta akilea watoto wengi wa ndugu zake kwa sababu mbali mbali takriban miaka 10 iliyopita. Picture Abel ambaye aliambatana na mkewe walitoa vifaa vya zahanati vikiwemo vitanda na madawa ambavyo kwa ujumla wake, vimegharimu fedha za kitanzania shilingu milioni 10. Hapa Gunta akimkabidhi Bi Manji msaada wa madawa huku mkewe Nana, ambaye aliambatana naye akishuhudia. Picture Picture Gunta pia alikabidhi fulana ambazo zitatumika kama sare baada ya masomo kwa watoto hao, hapa akishiriki katika kuwakabidhi watoto wenyewe. Kituo hicho kilichopo Mkuranga, Mkoa wa Pwani kina watoto 61 wanaoishi hapo huku 48 wakiwa wanasoma za msingi zilizopo wilayani Mkuranga, saba shule ya Sekondari na waliobaki wakiwa hawajafikia umri wa kwenda shule. Picture picha ya pamoja Chuo kinakabiliana na changamoto mbali mbali katika kipindi hiki ambacho bado hawajakuwa na miradi ya kujiendesha, vitu kama mavazi, chakula, ada za watoto ambao wanasoma nje ya Kituo, na waalimu wa kujitolea kuwafundisha watoto masomo ya ziada baada ya saa za masomo. Kufuatia hilo unakaribishwa kutembelea Kituo na kujionea mwenyewe hali halisi na kutoa chochote utakachojisikia iwapo utahamasika. Namba ambayo unaweza kupiga pia ili kupata maelekezo zaidi ni +255 655 786 011 Unaweza kusaidia wanakituo hawa kupitia akaunti ya KBC namba 3300828357. --- Picha, Maelezo, shukurani kwa: Henry Mdimu wa mdimuz.blogspot.com Add Comment Picha za hafla ya akina-Mama wa DMV ya kumuaga Balozi Mwanaidi Sinare-Maajar 28/01/2013 0 Comments WkinaMama waishio DMV - Marekani walishirikiana pamoja kuaanda hafla ya chakula cha usiku pamoja na muziki, mahsusi kwa ajili kumuanga Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nchi za Marekani na Mexico, Mhe. Mwanaidi Sinare- Maajar. Hafla hiyo ilifanyika siku ya Jumamosi Jan 26, katika ukumbi wa Greenway Center uliopo Greenbelt, Maryland. Zifuatazo ni picha za muhtasari halfa hiyo kutoka wa Abou Shatry wa SwahiliVilla Add Comment Zanzibar: UN yaendesha mafunzo kuhusu shughuli za UNDAP na Haki za Binadamu
Katibu wa Chama cha wanasheria wanawake Zanzibar Hamisa Mmanga Makame akitoa somo katika mafunzo hayo ambapo amezungumzia masuala y...
Kikao cha Wanamtwara na Waziri Mkuu - Dondoo za yaliyojiri (audio)
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akisisitiza jambo wakati wa kikao chake na Baadhi ya Viongozi wa Vyama vya siasa na viongozi wa Asasi ...
Elizabeth Michael ‘Lulu’ apata dhamana
Lulu) akizungumza na wakili wake Peter Kibatala muda mfupi kabla ya kuanza kusikilizwa ombi lake la dhamana leo asubuhi (picha: Raha za ...
Kikwete akiri tatizo la ajira kwa vijana kuwa 'bomu' linaloweza leta machafuko...
Peter Saramba na Mussa Juma, Arusha | Mwananchi RAIS Jakaya Kikwete amekiri kuwa ukosefu wa ajira kwa vijana ni tatizo kubwa na kwamba l...
Kauli ya @ZittoKabwe kuhusu yanayoendelea Mtwara; Ref. Taarifa ya Ikulu
TAARIFA YA NDUGU ZITTO KABWE (MB) KUHUSU YANAYOENDELEA MTWARA NA MRADI WA BOMBA LA GESI ASILIA Serikali iache kutafuta mchawi, iende M...
Ujumbe wa kuadhimisha leo Siku ya Ukoma Duniani
Jikabidhi kabisa kwa Mungu, atakutumia kutimiza mambo makuu kwa hali ambayo utaamini zaidi kwamba ni Upendo wake dhidi ya Udhaifu wako. ...
White peacocks
My auntie's friend, Chloe posted these photos of white peacocks on her Facebook wall. They were take at the Green Pastures ...
Tamko la Makanisa ya PCT Mtwara kuhusu Gesi ya MnaziBay
Baada ya kufuatilia kwa undani, na kwa upana kuhusu swala la gesi ambalo linaendelea kuwa ni mgongano au, ni mgogoro kati ya Serikali na ...
MAELEZO KAMILI KUHUSU PICHA YA RECHO,LINAH NA DIAMOND HAYA HAPA.
Jana kupitia mitandao ya jamii, kulikua na mzunguko wa picha hii kila kona ya mitandao hiyo, huku ikiwaacha mashabiki kujiuliza maswali m...
IRAMBAHOI IPO BIN TAABANI KIELIMU, MATOKEO YA DARASA LA SABA( 2012 )
>>> ILIKUWA YAA MWISHO KIMKOA, HATA MWAKA 2011 >>> HAIKUTOA MWANAFUNZI WA KIPAJI HATA MMOJA >>> IL...
Meya @JerrySilaa: Mgeni rasmi katika mahafali ya Kidato cha VI Sekondari ya Azania
Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Azania wakiwa wamejipanga kumpokea mgeni rasmi katika mahafali ya kidato cha Sita ya ...