Katibu wa Chama cha wanasheria wanawake Zanzibar Hamisa Mmanga Makame
akitoa somo katika mafunzo hayo ambapo amezungumzia masuala ya Haki za
Binadamu, umuhimu wa kuzingatia jinsia na wajibu wa vyombo vya habari
katika kuleta usawa.
Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin akielezea mada ya umuhimu wa
mawasiliano kwa maendeleo na kuwataka wamiliki wa vyombo vya habari na
serikali kwa ujumla kubadilisha sera zinazosimamia vyombo hiyo ili
ziweze kutoa fursa kwa waandishi kuwa huru katika uandishi na kuripoti
habari bila kubanwa.
Meza Kuu Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu Zanzibar
Hassan Khatibu, Mratibu wa FAO Ofisi ya Zanzibar Ali Haji Ramadhan,
Mwakilishi wa mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa Zanzibar Anna Senga,
Mwezeshaji wa mafunzo hayo mwandishi mkongwe Salim Said Salim na
Mwenyekiti wa UNCG Yusuph Al Amin.
0 comments:
Post a Comment