Mamlaka ya Hali ya Hewa
Tanzania, TMA, inauhadharisha umma kuhusu hatari ya uwezekano wa kuwepo
kwa mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo nchini kutokana na
kimbunga “FELLENG”.
Baadhi ya maeneo ya mikoa ya Rukwa, Iringa, Mbeya, Njombe, Ruvuma, Morogoro, Pwani, Lindi, Mtwara na maeneo jirani ya mikoa hiyo huenda yakapatwa na mvua kubwa (zaidi ya milimita 50 katika kipindi cha saa 24 kila siku) kati ya tarehe 30 Januari, 2013 hadi 01 Februari, 2013.
Kimbunga “FELLENG” cha Kaskazini-Mashariki mwa Madagascar kinavuta upepo wenye unyevunyevu kutoka Congo kupitia maeneo tajwa. Mamlaka inaendelea kufuatilia hali hiyo.
Tafadhali tizama picha ya satelite na kusoma taarifa kamili ya hali inavyoonekana wakati taarifa hii ikitolewa.

0 comments:
Post a Comment