Friday, October 19, 2012

Post hii itakuwa inahaririwa mara kwa mara na kuongezwa taarifa mpya (UPDATES) kadiri zinavyopatikana, ya ripoti kutoka vyanzo mbalimbali za vitendo vinavyoashiria vurugu katika maeneo ya Tanzania.

** Tafadhali “scroll” kuelekea chini ya ukurasa huu, ili kuona taarifa mpya (update).

---

Taarifa zinafahamsiha kuwa zimezuka vurugu katika maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam, ambapo baadhi ya watu wanaandamana kuelekea Kidongo Chekundu hali iliyowalazimisha Polisi kutumia mabomu ya machozi kuzuia maandamano hayo.

Vile vile, Polisi wamelazimika kutumia helikopta ili katika harakati za kuzuia vurugu hizo.
Picture
photo via Uncle Fafi @Tanganyikan (credit)

AGIZO LA POLISI: MARUFUKU KUANDAMANA DAR

Agizo limepatikana via blogu ya John  Badi

Viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dar es Salaam wamekutana na kutoa tamko la kuzuia Waislamu kuacha kuandamana mara moja.

Katika taarifa ya waliyoitoa mapema leo asubuhi wakuu na viongozi mbalimbali wa Serikali wakiwemo wa dini wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadick, aliwatoa hofu wananchi wa Jiji la Dar es Salaam kuendelea na shughuli zao kama kawaida kwani wamejipanga kulinda hali ya amani.

Akitoa tamko hilo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa kumekuwapo na taarifa za waumini wa Kiislamu kuandamana na kufanya fujo mara baada ya swala ya Ijumaa na baadala yake amewataka kuacha kufanya hivyo na warejee majumbani kwa amani na suala hilo linashughulikiwa kisheria.

Hata hivyo kwa upande wao viongozi wa dini waliokutana na Mkuu wa mkoa  juu ya kutolea tamko hilo waliwaasa waumini wote kutoingia mitaani na kuandamana kwani wakifanya hivyo ni kukiuka misingi mbalimbali  ya kisheria iliyopo kihalali na watakapofanya hivyo ni kukiuka sheria za nchi.

Kamanda Kova, Sheikh wa mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Musa bin Salum amewataka wakuu wa misikiti mkoa wa Dar es Salaam kuwakataza waumini hao kufanya maandamano kwani kufanya hivyo ni kukiuka misingi iliyopo. Aidha, aliwaomba waumini warejee majumbani  kwa amani.

Askofu  Makunda aliwataka watanzania kuendelea kufuata misingi ya kiimani bila chuki wala kufanya fujo.

Kamanda wa Polisi Kanda maalum mkoa wa Dar es Salaam, Suleiman Kova alitoa onyo kali kwa waislamu kuacha kufanya hivyo hii leo kwani kwa atakaekiuka atachukuliwa hatua kali. Kova aliwataka waumini kurejea majumbani mwao kwa amani bila kufanya maandamano  na pia aliwataka wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuendelea na shughuli zao kama kawaida na kupuuza tishio hilo la fujo kutoka kwa waislamu.

“Jeshi limejipanga kuakikisha hali ya amani na usalama inakuwepo hivyo taadhari kwa waislamu kuacha kufanya maandamano mara moja” alisema Kova kwenye kikao hicho ambacho kinaendelea hivi sasa.

Wakuu hao wamekutana kwa dharura baada ya kuwepo kwa taarifa za juu ya waumini hao kutishia kuandamana  na kufanya fujo.
Picture
Kariakoo (picha: Janeth Stephano via facebook.com)
Taarifa kutoka kwenye blogu ya “Habari Mseto”

DAR ES SALAAM, Tanzania

Vurugu kubwa zimetokea mchana huu katika maeneo yanayozunguka eneo la Kariakoo na kusababisha hofu kubwa na Polisi wamelazimika kutumia mabomu ya machozi na kutawanya mikusanyiko ya watu waliokuwa wamejiandaa kuandaamana kuelekea katika Ikulu ya Magogoni jijini.

Maduka yote katika maeneo hayo yamefungwa na shughuli mbalimbali zimesimama pamoja na Ofisi mbalimbali zimefungwa kutokana na hofu kubwa iliyotanda.

Kwa mujibu wa matangazo ya moja kwa moja ya Redio One wananchi wanakimbizana hovyo kukimbia mabomu ya machozi yaliyokuwa yakipigwa na Polisi kuwatawanya waumini waliokuwa wakitoka msikitini.

Hata hivyo taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, waumini hao wameweza kutawanywa na hali bado tete huku magari ya jeshi la Polisi yakielekea katika maeneo ya Kinondoni ambapo kunadaiwa kuwa hali si shwari na vurugu kama hizo zinaendelea.

Na habari zilizotufikia sasa hivi Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limepeleka vikosi vyake katika maeneo ya Kariakoo ambapo vurugu zimekuwa kubwa ili kutuliza hali ya uvunjifu wa amani. 
Picture
Picha hii imepigwa mcha huu katika mtaa wa Mkwepu jijini Dar es Salaam leo, hali bado ni tete kufuatia maandamano ya waislamu, mitaa kadhaa yenye pilika pilika za watu leo imekuwa mitupu kufuatia hofu kubwa iliyojitokeza. (picha, maelezo: Francis Dande “Habari Mseto” blog)
Picture
Picha ya Posta @lijocha
Picture
picha via Jiji la Dar blog
Picture
Ikulu upande wa baharini (photo-tweet @Irenei2011)
Picture
Polisi wamefunga barabara ya hapa Posta Mpya na daladala zinageuza hazitumii tena kituo cha kawaida. (picha: JamiiForums.com)
Ujumbe wa simu kutoka kwa mtu wa karibu:

      “Kuna taarifa kuwa Polisi wamelazimika kulipua mabomu katika maeneo ya Kariakoo na Chang'ombe ili kuwatawanya waandamanaji. Mimi kwa sasa nipo maeneo ya Mikocheni. Hapa nilipo hamna vurugu
Picture
“Imagine hiyo ni Posta Mpya sasa hivi (saa tisa alasiri) hakuna magari yanayoingia” (picha na ujumbe kutoka kwa rafiki aliyepo eneo hilo)
Picture
Eneo la kati, jijini Dar es Salam (picha: Dkt. V. Mahamba)

*Ikiwa Serikali haijaliona tamko, hili, natumai kwa kuliweka hapa tayari takuwa imeliona*

0 comments:

Post a Comment