Mwanafunzi wa Kidato cha Kwanza katika Shue ya Secondari ya Chamriho
iliyoko wilayani Bunda mkoani Mara amefariki dunia baada ya kupigwa na
radi huku wenzake watatu wakinusurika.
Radi hiyo pia imeiteketeza kwa moyo nyumba walimokuwemo vijana hao.
Tukio hilo ambalo limeleta maafa na kuacha makubwa, limetokea katika kijiji cha Nyang’aranga katika kata ya Mugeta majira ya saa tatu usiku wakati marehemu na wenzake walipokuwa wakijisomea ndani ya nyumba hiyo.
Afisa mtendaji wa kijiji hicho, Fikiri Magunila amemtaja mwanafunzi aliyepigwa na radi kuwa ni Karosi Joram aliyekuwa akisoma kidato cha kwanza katika Shule hiyo.
Kumekuwepo na matukio ya radi kali katika kijiji hicho ambapo miaka ya hivi karibuni radi iliua watu wawili.
---
Habari hii imeandikwa na Pascal Buyaga - Bunda, Mara.
Imewasilishwa na Magiri Paul wa wotepamoja.com

0 comments:
Post a Comment