MrokiM blog -- Mtu mmoja anadaiwa kufa kwa kupigwa risasi kichwani huku wengine kadhaa wakijeruhiwa vibaya kwa Risasi za moto baada ya Polisi kuwarushia Risaasi za moto na mabomu ya machozi waandamanaji wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mjini Morogoro.
Polisi waliwatawanyisha wanafuasi hao walipokuwa wakifanya maandamano maeneo ya Msamvu mjini Morogoro mchana wa leo. Polisi walitibua maandamano hayo waliyodai hayakuwa rasmi, kwa kutumia mabomu ya machozi.
--- ENDS ---
Lukwangule blog -- POLISI Mkoani Morogoro wameingia kwenye marumbano na Chadema baada ya kutokea kwa mauaji ya kijana Ally Shana Zone wakati wa maandamano ya CHADEMA mkoani hapa.
Kifo hicho kilichotokea majira ya mchana kimedaiwa kusababishwa na risasi na Polisi wakati wa purukushani za kuzima maandamano ya Chama hicho leo.
Pia imedaiwa katika purukushani hizo, Frank Valimba na Hashimu Seif walijeruhiwa sehemu mbalimbali za miili yao.
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Slaa, alisema katika mkutano wa hadhara eneo la Uwanja wa Ndege Mjini hapa kuwa amewateua viongozi wanne wakiongozwa na Mbunge Tundu Lissu, pamoja na Mwanasheria, Amani Mwaipaja kukutana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Faustine Shilongile kuangalia kwa undani mazingira ya kifo cha kijana huyo.
Chadema baada ya kuzungunza na Viongozi wa Polisi, wamekubaliana Mwili wa kijana huyo uhifadhiwe chumba cha Maiti cha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ili kupicha uchunguzi wa kitaalamu kubaini chanzo cha kifo hicho.
Kwa mujibu wa Tundu Lissu, Uongozi wa Polisi umeamua kupata Daktari aliyetajwa kwa jina moja la Dkt. Mataka ili kuenndesha uchunguzi huo ambapo Mwanasheria wa CHADEMA-Morogoro, Amani Mwaipaja atasimamia shughuli hiyo.
Lissu aliwataka wanachama wa Mkoa wa Morogoro walioshuhudia kijana huyo akipigwa mabomu ama risari wanatakiwa kujitokeza kutoa ushuhuda wakati wa uchunguzi wa kimahakama ili kudhibitisha kifo hicho kuwa ni cha mkono wa mtu.
Baadhi
ya wafuasi na wanachama wa Chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA
mkoani Morogoro wakiongozwa na polisi baada ya kuwatawanyisha walipokuwa
wakifanya maandamano maeneo ya Msamvu mjini Morogoro mchana wa leo.
Polisi walitibua maandamano hayo yanayodaiwa kutokua rasmi kwa mabomu ya
machozi. (picha Father Kidevu blog)
Mkuu
wa Operesheni Sangara-Vuguvugu la Mabadiliko (M4C) BENSON KIGAIYA akiwa
chini ya ulinzi wa gari la polisi mara baada ya kukamatwa wakati wa
zoezi la kuwapokea viongozi wa juu wa chama hicho kushindikana katika
eneo la Msamvu kwa ajili ya maandamano kuelekea kwenye mkutano wa
hadhara wa CHADEMA shule ya msingi Uwanja wa Ndege mkoani Morogoro.
(picha : Juma Mtanda)
Msimamo wa JOHN MNYIKA kuhusu vurugu, risasi, kujeruhi na “kuua” Morogoro!
Niliwahi kutahadharisha baada ya tukio la Dkt Stephen Ulimboka kuwa serikali imeanza kutumia mbinu haramu kudhibiti fikra mbadala, CCM imeanza kuongoza serikali kiimla na ipo siku umma utafikia hatua ya kukiona kama chama cha mauaji.
Raia watatu wasio na hatia wamefyatuliwa risasi na mmoja amefariki. Haya yamefanyika kwenye maandamano ya amani ya wananchi kuwapokea viongozi wa CHADEMA kuelekea kwenye mkutano. Vurugu zimeanzishwa na polisi kwa mujibu wa mashuhuda wa ushahidi wa video.
Vyanzo vyangu vinaniambia sasa wameagiza gari tatu za FFU na gari za kuwasha toka Dar Es Salaam. Tuombe MUNGU wasiamue kuvuruga mkutano wa hadhara ambao wananchi wamekusanyika kwa wingi hivi sasa.
States captured by grand corruption of the ruling party cronies for so many years resorts to bullets as a way of stopping M4C through the ballot. Maisha ya wachache yako mashakani lakini si mabadiliko kwa maslahi ya wengi.
Source: wavuti
0 comments:
Post a Comment