Kikundi cha wanawake walioitikia mgomo huo
Isabelle Ameganvi ndie anaehamasisha mgomo huo wa Kusitisha huduma ya Ngono kwa mda wa wiki nzima.
Raisi wa Togo Faure Gnassingbe anaeshinikizwa kujiuzuru madaraka kwa njia ya SEX STRIKE.
Kikundi cha wanaharakati wanawake mjini Lome,nchini Togo kimeshawishi
Wanawake wenzao kuwepo kwa Mgomo wa wiki moja wa kufanya tendo la ndoa
iwe kwa Waume au wapenzi wao ,ikiwa ni hatua ya kushinikiza Kungo'ka kwa
raisi aliepo madarakani Raisi Faure Gnassingbe.
Akizungumza na waandishi wa habari kiongoziwa kundi hilo la wanaharakati
linalojiita Let's Save Togo mama Isabelle Ameganvi amesema kwa mgomo
huo anaamini wanaume wa nchi hiyo watachukua atua na kumuweka katika
wakati mgumu Rais huyo..Ameganvi ambae ni mwanasheria amesema kua Kundi
lake hilo linafata mfano wa wanawake wa Liberia ambao walitumia mgomo
kama huo wa Ngono mwaka 2003 kupigania Amani nchini kwao.
“We have many means to oblige men to understand what women want in Togo,”
Gnassingble ambaye yupo madarakani toka 2005 akichukua nafasi ya Hayati
baba yake Eyadema Gnassingble alie tawala Afrika Magharibi kwa kipindi
cha miaka 38,mpaka sasa hajaongea chochote kuhusiana na mgomo uo ata
mkewe alkadhalika. Ingawa mpaka sasa imeripotiwa tayari raia zaidi ya
100 wamekamatwa kufuatia mgomo huo.
Ata hivyo katika hatua nyingine baadhi ya wanawake wamonekana kuhofia
mgomo kwani inaonyesha waume zao wanapenda sana kufanya tendo hilo na
wanaweza hatarisha ndoa zao.
“I do agree that we women have to observe this sex strike but I know my
husband will not let me complete it. He may agree at first, but as far
as I know him, he will change overnight,” alisema Judith Agbetoglo “So I
don’t believe I can do the one-week sex strike. Otherwise, I will have
serious issues with him. He likes that too much.”
Pia ata baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wameonyesha kua zoezi
hilo wamefanya kwa wiki nzima ni siku nyingi sana nakushauri walau
ngekua mgomo wa siku mbili tu.“One week sex strike is too much,” alisema Fabre wa The National Alliance for Change, ambae aliposhauri siku za kugoma kutoa huduma hiyo kundi la watu walio kuwepo kwnye demonstration hiyo wacheke saana“Let’s go for only two days” alimaliza Fabre
Kanakwamba haitoshi wengine walienda upande wa pili wakimponda kiongozi wa mgomo huo Isabelle Amegamvi kua anaona rahisi kushawishi wenzake kwasababu yeye hana mme nyumbani kwake.Na ata hivyo hakuna anaeweza kujua au kuzuia kinachoendelea faragha wapenzi wakiwa pamoja!?.
“It is easy for her to say because she is not married herself. She does not live with a man at home,” alisema Ekoue Blame, ambae ni mwandishi wa habari wa Togo “Does she think women who live with their husband will be able to observe that? By the way, who controls what couples do behind closeddoors?” alimaliza Blame.
Inaonyesha hawa jamaa wanapenda sana huu mchezo yaani wiki ni nyingi kwao kiasi hiki.
Na je inakuaje kama Tanzania tukitumia staili hii kushinikiza kitu flani kwa Serikali.Unafikili itawezekana
0 comments:
Post a Comment