Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Nyamagana mkoani
Mwanza kwa kushirikiana na baadhi ya viongozi waandamizi wilaya ya
Ilemela kimefanya maandamano ya amani kwa lengo la kumpongeza Rais
Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa tarehe 01/07/2012 iliyokuwa na taarifa
kuhusu mgomo wa Madaktari nchini.
Risala ya Chama hicho iliyowasilishwa na katibu wake Mwenezi wilaya ya Nyamagana Dkt. Elirehema Moses Kaaya imewasihi Madaktari wote warudi kazini mara moja ili kuendelea kuwahudumia Watanzania.
Dkt. Kaaya amesema kuwa ni kweli madai ya madaktari yana mantiki kubwa, hasa ukizingatia ugumu na mazingira wanayofanyia kazi, hata hivyo Serikali kwa kiwango kikubwa imejitahidi kutekeleza baadhi ya matakwa yao.
Bofya picha zilizopachikwa hapo kuzikuza ili kuweza kusoma ujumbe uliopo kwenye mabango.

0 comments:
Post a Comment