Mfanyabiashara aliyetambulika kwa jina la Joseph Ngisha (24) mkazi
wa Sakina, Songambele, jijini Arusha anashikiliwa na polisi kwa kosa
la kumuoa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 8 kinyume cha sheria
kwa mahari ya ng'ombe wanne.
Kwa mujibu wa Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Liberatus Sabas, polisi pia inamshikilia baba mzazi wa mtoto huyo, Lemomomo Olokuto (42) mkazi wa Mto wa Mbu kwa tuhuma za kumwoza mtoto wake tangu mwaka 2010 akiwa na miaka 8 (sasa hivi mtoto huyo ana umri wa miaka 11.)
Alisema Ngisha alitiwa mbaroni Julai 18, mwaka huu majira ya saa 3.45 asubuhi nyumbani kwake baada polisi kupata taarifa za siri na kumkuta akiishi na mtoto huyo huku akiwa amembebesha ujauzito wenye umri wa miezi mitatu.
''Ngisha alipohojiwa na polisi alikiri na kueleza kuwa yeye alitoa mahari ya ngómbe 4 badala ya 3 waliotajwa na baba mkwe wake'' alisema.
Kamanda Sabas alifafanua kuwa Ngisha alianza kumchumbia mtoto huyo baada ya kuacha kunyonya kwa mama yake na kwamba alipofikisha umri huo aliwafuata wazazi wake na kuwaeleza nia ya kutaka kumchumbia.
Hata hivyo, mzazi wa upande wa mama aligoma huku baba yake ambaye ni mtuhumiwa akiruhusu mtoto wake aolewe bila kupingwa.
Aliongeza kuwa, mtuhumiwa Ngisha baada ya kuona mama mzazi akipinga mtoto wake asiolewe, alimrubuni kuwa anakwenda kumsomesha shule, kitendo ambacho hakukifanya na badala yake alikuwa akimwingilia kimapenzi na kumfanya kama mkewe.
Kamanda alisema kuwa taarifa za mtuhumiwa kuishi na mtoto huyo kama mke ziligunduliwa na majirani kwani mara nyingi alikuwa akimfungia ndani bila mtu kujua huku akiwaeleza baadhi ya jamaa zake kuwa ni mdogo wake.
Aidha, alisema kuwa kwa sasa mtoto huyo yupo chini ya uangalizi wa ofisi za ustawi wa jamii jijini Arusha, ambapo anachunguzwa kiwapo atakuwa ameathirika na magonjwa ya zinaa ama la.
Alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mtoto huyo ameathiriwa kwa kupata ujauzito wa miezi mitatu ambapo kulingana na umri wake ni vigumu kuhimili maisha ya kuitwa Mama.
Baba wa mtoto huyo alipoulizwa alikiri kumwoza mtoto wake kwa mahari ya ngómbe watatu tofauti na idadi inayotajwa na mkwewe Ngisha.
Uchunguzi wa awali kutoka ndani ya jeshi la polisi unaonyesha kuwa Ngisha alimchukuwa mtoto huyo tangu mwaka 2010, hata na hivyo alipohojiwa kwa mara ya kwanza aklikataa kosa hilo hadi siku ya jana ambapo alikiri kutenda kosa hilo.
Sabas alisema kuwa kufuatia tukio hilo, baba mzazi anashikiliwa na kumuunganisha na Baba mkwe wake, na kwamba wote wawili watafikishwa mahakani kujibu tuhuma zianzowakabili baada ya jeshi la polisi mkoani Arusha kukamilisha uchunguzi wake kuhusiana na tukio hilo.

0 comments:
Post a Comment