Mshauri wa CHADEMA ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam, Dkt. Kitila Mkumbo, amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya
Hakimu Mkazi ya mjini Singida akikabiliwa na tuhuma za kutoa lugha ya
matusi kwa mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba (CCM).
Dkt. Mkumbo ameunganishwa katika kesi hiyo pamoja na ofisa wa sera na utafiti wa CHADEMA Mwita Mwikwabe (37) ambaye alisomewa pia shitaka hilo Julai 16mwaka huu.
Awali Mwanasheria wa serikali, Maria Mudulugu alidai kwamba Julai 14 mwaka huu, saa 10 jioni, mshtakiwa huyo alitoa lugha ya matusi kwa Mwigulu kuwa ni malaya na mzinzi huku akijua wazi kwamba kitendo hicho ni kinyume cha sheria.
Mbele ya Hakimu wa Mahakama hiyo, Ruth Masamu, mwanasheria huyo alidai kuwa mshtakiwa alitoa lugha hiyo ya matusi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya kituo cha mabasi Kijiji cha Nguvumali, Kata ya Ndago.
Dkt. Mkumbo alikana shitaka hilo na yupo nje kwa dhamana hadi Julai 30 mwaka huu, kesi hiyo itakapotajwa tena.
Nao wakazi wawili wa Kijiji cha Nguvumali, Kata ya Ndago, Paulo Nashokigwa (27) na Emanuel Shila (24), wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya mjini hapa wakikabiliwa na tuhuma za kushiriki kumuuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Yohana Mpinga (30).
Mwanasheria huyo wa serikali alidai kuwa Julai 14 mwaka huu, saa 10 alasiri katika Kijiji cha Nguvumali, Kata ya Ndago, washtakiwa wote kwa pamoja wakitumia fimbo na mawe, walimpiga Yohana na kumsababishia kifo.
Washtakiwa hao hawakutakiwa kujibu lolote kwa vile Mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji. Na wameunganishwa na washtakiwa wengine 12 waliosomewa shitaka lao la mauaji Julai 16 mwaka huu, kesi hiyo itatajwa Julai 30 mwaka huu.

0 comments:
Post a Comment