Ni vizuri sana kwako kuweza kujua aina ya ngozi yako maana itasidia wewe
uweze kuitunza ngozi yako vizuri.Vile vile itakusaidi katika kujua ni
vipodozi vya aina gani utumie kutokana na ngozi yako.
Hakuna ngozi mbili ambazo zinafanana exactly ila zinatofautiana ambapo
inawezekana ngozi yako ikawa ni Ngozi Kavu, Ngozi ya Kawaida, Ngozi ya
mafuta na ngozi mchanganyiko yaani combine skin.
Ili kujua ngozi yako ni ya aina gani osha uso wako kwa kutumia sabuni ya
kusafishia uso then baada ya dakika 30 chukua tishu na futa sehemu ya
paji lako la uso, kwenye pua, kidevu na mashavu.
Kama tishu hiyo haitaonyesha kuwana mafuta baada ya kufuta basi ngozi yako itakua ni aina ya ngozi kavu.
Ngozi kavu huwa inaonekana rough na hukabiliwana mistari na wrinkles
lakini kama ngozi yako kuna sehemu nyingine inakua kavu sehemu nyingine
inakua na mafuta basi ngozi yako itakua ni ngozi mchanganyiko.
Ngozi ya kawaida au Normal skin huwa inaonekana laini na ngozi hii ya
mafuta ukiigusa unayahisi mafuta na huwa inang`aa. Ngozi hii ya mafuta
huwa inakabiliwa sana na blackheads na pimples/chunusi na kwa kuwa ngozi
hii ni sensitive inahitaji special care na umakini na vipodozi
unavyopaka kwenye uso wako.
Kwa watu wenye ngozi sensitive kama hii ni lazima kutumia misaada ya
ushauri kwa wataalamu wa ngozi ili kulinda ngozi zao kupata
mzio/allergic. Ni lazima mara kwa mara uwe na utaratibu maalum wa
kuihudumia ngozi yako kulingana na mahitaji ya ngozi yako na huenda
ikachukua muda mrefu kwa ngozi yako kurudia hali ya kawaida kuweza
kuondokana na hili tatizo.
kazi ni kwako
ReplyDelete