“HII sasa ni kufuru!” Hivi ndivyo utakavyoweza kusema kwa Davies Mosha ambaye ni makamu mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga, ambaye nafasi yake kwa sasa klabuni hapo inashikiliwa na Clement Sanga.
Kwa tafsiri ya haraka, yawezekana Mosha anaweza kuwa ndiye kiongozi pekee wa soka nchini kumiliki gari la kifahari na lenye gharama kubwa aina ya Lamborghini kama ambalo linamilikiwa na mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.
Mosha ameliambia Championi Ijumaa kuwa anamiliki magari kadhaa ya kifahari kwa matumizi yake binafsi na familia yake.
Ameinunua kwa bei gani?
“Kutokana na ubora wa gari hili, nililazimika kutoa shilingi bilioni moja kwa ajili ya kulinunua, kama unavyojua ni fedha nyingi, nimenunua kwa mapenzi yangu.
Alipolinunua
“Hili gari kaniuzia mtoto wa Bakhresa (Yusuph), baada ya kufikia makubaliano kati yake na mimi, aliniuzia Julai 2011.
Spidi ya gari
“Hili gari kasi yake ya mwisho ni 360, ni kasi kali na inatosha kwa matumizi yangu binafsi.
Matumizi ya mafuta
“Matumizi ni ya kawaida wala siyo ya kuogopesha sana, inategemea na umbali utakaotembea.
Usumbufu anaoupata
“Usumbufu mkubwa ninaoupata kiukweli, nikiwa naendesha barabarani, madereva wengine wanalishangaa sana, hali inayosababisha kutokea ajali au msuguano mara kadhaa.
“Hivi karibuni dereva mmoja aliigonga sehemu ya tairi la nyuma kushoto kutokana na kuishangaa, ilikuwa maeneo ya Masaki hapahapa Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.