- Nani anasema Watanzania ni masikini sana? Ripoti iliyotolewa na Tanzania Communications Regulatory Authority (TCRA) inaonyesha kwamba kati ya Julai na Septemba mwaka jana, Watanzania walitumia jumla ya shilingi bilioni 555 (sawa na dola za Kimarekani milioni 396!) kwenye simu. Hii ni sawa na shilingi bilioni 185 kwa mwezi.
- Ripoti hiyo inaonyesha kwamba kuna watumiaji wa simu wapatao 20,771,487 nchini Tanzania na kwamba katika kipindi hicho cha miezi mitatu kila mtumiaji alitumia shilingi 26,724 kwenye simu.
- Kampuni ya Vodacom ndiyo inaongoza kwa kuwa na watumiaji wapatao 8,426,097 ikifuatiwa na Airtel (5,901,634), Tigo (4,575,534), Zantel (1,586,516), TTCL (256,064) na SasaTel (23,071)
- Kama vile mdau mmoja alivyodai, hapa bado hujaongeza bajeti ya bia na michango ya harusi. Pengine ni kweli kwamba tatizo letu siyo umasikini bali ni kushindwa kuelekeza nguvu zetu katika mambo ya msingi. Uboreshaji wa njia za mawasiliano hususani simu na mtandao ni hatua nzuri katika kujiletea maendeleo hasa kama zitatumiwa vizuri na kwenye mambo yanayohusu maendeleo. Inabidi sasa tukaze macho vijijini ambako ndiko waliko wananchi walio wengi. Kwa hakika takwimu hizi za TCRA zinafikirisha!
0 comments:
Post a Comment