MAREKANI
imeungana na Uingereza kushinikiza kutambuliwa kwa haki za mashoga,
ikitumia rungu la misaada yake inayotoa kwa nchi mbalimbali duniani,
huku ikitenga Dola za Marekani 3 milioni sawa na Sh5.1bilioni, kwa ajili
ya kufanikisha mkakati huo.
Shinikizo
hilo la Marekani ambalo ni taifa kubwa kiuchumi duniani, linazidi
kuchochea mjadala ulioibuliwa na Waziri Mkuu wa Uingereza, David
Cameron, ambaye alitangaza katika mkutano wa Jumuiya ya Madola
uliofanyika Uswis hivi karibuni kwamba, nchi yake itasitisha misaada
kwa nchi zote duniani ambazo hazitambui haki za mashoga.
Baada
ya Cameron, Rais Barack Obama wa Marekani naye juzi alitangaza kwamba,
taifa hilo kubwa litatumia uwezo wake wote ikiwamo misaada inayotoa
kwa nchi mbalimbali kuhakikisha haki za mashoga zinatambuliwa na
kuthaminiwa duniani.
Rais
Obama alitoa msimamo huo jijini Washington katika hafla ambayo pia
ilihudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Nchi hiyo , Hillary Clinton
ambaye ndiye alikuwa mzungumzaji mkuu.
“Wengine
wanasema kuwa haki za mashoga na haki za binaadamu ni vitu tofauti na
havifanani, lakini ukweli ni kwamba ni kitu kimoja na chenye
usawa,”alisema Clinton wakati akisoma taarifa hiyo maalumu yenye baraka
za Obama.
0 comments:
Post a Comment