SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema kuanzia sasa litaanzisha
utaratibu wa kuwakatia bima ya afya michezoni wachezaji watakaoitwa
kuunda kikosi cha timu ya Taifa (Taifa Stars).
Uamuzi huo ambao ni
sehemu ya mkakati kuwatia hamasa wachezaji na kuwajengea uwezo wa
kujituma, umekuja siku chache tangu Stars iibuke na ushindi wa mabao 2-1
dhidi ya Gambia katika mchezo wa kuwania kucheza Fainali za Kombe la
Dunia 2014.
Rais wa TFF, Leodegar Tenga aliwaambia waandishi wa
habari jana jijini Dar es Salaam kuwa, msingi mkuu wa hatua hiyo pia
unalenga kutoa fursa ya kupatiwa matibabu mazuri wachezaji wa Stars
wanapopata matatizo ya afya.
Tenga alisema anaamini ili mchezaji
aweze kuiwakilisha vizuri nchi yake, suala la afya bora na matibabu ya
uhakika anapopata matatizo ni mambo yasiyokwepeka kutekelezwa.
Aidha,
katika kuwaongeza hamasa na kujituma kusaka ushindi, kuanzia sasa
wachezaji watakuwa wanapata asilimia 15 ya mapato ya uwanjani, asilimia 7
iwapo watatoka sare na hawatapata kitu wakipoteza mchezo.
"Kiini cha
uamuzi huu ni kuwaongezea hamasa vijana wetu, na TFF itaendelea
kuwajengea mazingira mazuri yatakayowafanya kucheza kwa kujituma kusaka
ushindi kwenye mashindano mbalimbali.
"Tunafahamu bado tuna kazi
kubwa mbele yetu na hata hapa tulipofikia ni baada ya kubadili mwelekeo
unaosisitiza nidhamu na uwajibikaji wa pamoja," alisema Tenga.
Aidha,
Tenga alisema TFF itajivika jukumu la kuwatafuta wataalamu mbalimbali
wa masuala ya maisha na saikolojia ili kuzungumza na wachezaji wa Stars
na lengo ni kuwawezesha kujiamini na kujitambua.
Kuhusu mchezo wa
ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Gambia, Tenga alisema: "Kwa hakika uwezo
walionyesha wachezaji unastahili pongezi kwa kuweza kucheza dakika 90
bila kuchoka tofauti na siku nyingine."
Pia alipongeza taswira ya
uzalendo iliyoonyeshwa na mashabiki wa soka walioshuhudia mechi hiyo ya
Stars kwa moyo wa shikamano uliotambua utaifa tofauti na hapo awali
ambapo baadhi walikuwa wakizomea.
Amewataka kuendelea kufanya hivyo katika mechi zote hata kama timu hiyo ikifanya vibaya sababu haiwezi kuwa inashinda kila siku.
Amewataka kuendelea kufanya hivyo katika mechi zote hata kama timu hiyo ikifanya vibaya sababu haiwezi kuwa inashinda kila siku.
"Ningeomba
na Jumamosi mjitokeze kwa wingi kuishangilia timu yetu ya taifa
wanawake (Twiga Stars) itakapocheza na Ethiopia," alisema bosi Tenga.
0 comments:
Post a Comment