Kaburi la marehemu Steven Kanumba.
Marehemu Steven Kanumba.
KATIKA hali ya kushangaza, msanii wa
filamu Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ hivi karibuni alinaswa mchana kweupe
kwenye kaburi la aliyekuwa swahiba wake, marehemu Steven Kanumba
lililopo Kinondoni jijini Dar, Ijumaa Wikienda limeinasa.
Siku ya tukio
Chanzo chetu cha kuaminika kilichoomba
hifadhi ya jina lake kilitutonya kuwa siku hiyo Ray alifika makaburini
hapo na kwenda moja kwa moja mahali lilipo kaburi hilo kisha kuliinamia
kwa dakika kadhaa huku akionekana mwenye jambo moyoni.
“Sisi tulikwenda pale kulifanyia usafi
kaburi la ndugu yetu. Mara tukamuona Ray akiingia na kwenda kwenye
kaburi la Kanumba, ni kama mtu aliyekuwa akimuombea dua hivi…,” alisema
mtoa habari huyo na kuongeza:
“Ninachojua mimi mpaka Kanumba anafariki, walikuwa kwenye bifu na sikumbuki kama liliisha ‘so’ huenda alifika pale kwa nia ya kumuomba msamaha ili huko alipo amsamehe.”
“Ninachojua mimi mpaka Kanumba anafariki, walikuwa kwenye bifu na sikumbuki kama liliisha ‘so’ huenda alifika pale kwa nia ya kumuomba msamaha ili huko alipo amsamehe.”
Rafiki yake atoboa
Hata hivyo kabla ya kuzipata taarifa
hizo, juzikati rafiki wa Ray ambaye naye aliomba hifadhi ya jina lake
aliliambia gazeti hili kuwa msanii huyo amekuwa akiumia sana kila
anapokumbuka bifu lake na marehemu.
“Jamaa kila anapokumbuka kuwa Kanumba kaondoka wakiwa bado hawajakutana na kusawazisha mambo, anakosa raha sana.
“Alisema ipo siku atakwenda kuongea na marehemu pale kaburini ili huko aliko ajue anaumia kwa hali hiyo,” alidai mtoa habari huyo.
“Alisema ipo siku atakwenda kuongea na marehemu pale kaburini ili huko aliko ajue anaumia kwa hali hiyo,” alidai mtoa habari huyo.
Ray anasemaje?
Katika kujua ukweli wa tukio hili,
mwandishi wetu alimtafuta Ray kupitia simu yake ya mkononi na
alipopatikana alikiri kufika kwenye kaburi la swahiba wake huyo.
“Ni kweli nilikwenda pale kwenye kaburi
la Kanumba kama ambavyo ndugu, jamaa na marafiki wamekuwa wakienda,”
alisema Ray kwa kifupi. Alipobananishwa kuwa inadaiwa kilichompeleka ni
kwenda kuomba msamaha kwa yale yaliyotokea kati yao enzi za uhai wake,
Ray alisema:
“Nilishaongelea mara kadhaa ishu ya tofauti yangu na marehemu kwamba mpaka anafariki dunia tulikuwa tupo sawa.”
Tujikumbushe Enzi za uhai wake, Kanumba
na Ray walikuwa kwenye bifu lakini baadaye ikadaiwa waliwasiliana kwa
simu na kuondoa tofauti zao licha ya kwamba hawakuweza kukutana uso kwa
uso mpaka umauti ulipomkuta.
SOURCE:Globalpublishers
Sorry bt Id like to advise u to check the grammer/structure of ya sentence jus below the digits which shows the number of visitors.....I think u meant "Translate to your language" and not "Translate to you are language"
ReplyDeleteThanks!