Naibu
Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene leo hii ameibuka
Bungeni wakati akijibu swali la Mbunge na kushangiliwa hali iliyomlazimu
Spika kuwaomba wabunge wampe muda ajibu swali aliloulizwa.Akijibu
alianza kusema''Mh.Spika makofi na kushangiliwa huko ni kudhihirisha
kwamba maneno yalikuwa yamezushwa mimi sihusiki kwani mimi ni mzima na
sijakatwa mikono kama mnavyoniona'' alisema Mh.Simbachawene.
Toka juzi kulizuka maneno kuwa akiwa huko Singida amefumaniwa na mke wa mtu katika nyumba ya kulala wageni wakati akiwa njiani kwenda Karatu kwenye msiba wa shemeji yake.
Toka juzi kulizuka maneno kuwa akiwa huko Singida amefumaniwa na mke wa mtu katika nyumba ya kulala wageni wakati akiwa njiani kwenda Karatu kwenye msiba wa shemeji yake.
0 comments:
Post a Comment