“Pamoja na vitu vyote, Maximo ameomba kuja na msaidizi wake
ambaye atafanya naye kazi pamoja na kila kitu kimekubaliwa. Hivyo klabu
yake ikukubali, atakuja na msaidizi wake katika timu hiyo anayoifundisha
na mazungumzo yanahusisha watu wote hao wawili.
Na Saleh Ally
KOCHA wa zamani wa timu ya taifa, Taifa Stars, Marcio Maximo
amekubali kuifundisha Yanga na imeelezwa usajili wa beki Kelvin Yondani
ni msisitizo wake kabla hajatua nchini.
Hivi karibuni mbele ya Rais
Jakaya Kikwete alipokuwa ziarani nchini Brazil, Maximo alisema hatarejea
kuifundisha timu ya taifa na alikuwa akiendelea kufanya kazi katika
klabu yake ya Democrata-GV ya Brazil.
Habari za uhakika kutoka ndani
ya Yanga zinaendelea, Maximo amekubali kwa asilimia 100 kuifundisha
Yanga na ameutaka uongozi wa klabu hiyo kufanya makubaliano na klabu
yake, iwapo atakubali, basi ataanza rasmi kazi ya kuinoa klabu hiyo
kwenye michuano ya Kombe la Kagame, au baada ya hapo.
“Maximo
amekubaliana na Yanga kwa kila kitu, suala la mshahara halina tatizo kwa
kuwa hauna tofauti na ule aliokuwa analipwa Kosta Papic. Hivyo Yanga
imekubali kumlipa na akifika tu atapewa mishahara ya miezi mitatu
kabisa.
“Kingine
atakachopewa ni gari nzuri ya kutembelea pamoja na nyumba katika eneo la
Masaki, Mikocheni au Msasani na kila kitu kipo tayari,” kilieleza
chanzo cha uhakika kutoka ndani ya Yanga. Mazungumzo kati ya klabu ya
Maximo na Yanga yameshaanza na inaonekana huenda mambo yakaenda vizuri
na kocha huyo akarejea nchini, safari hii akiwa katika ngazi ya klabu.
Katika
mkataba wake wa mwanzo akiwa na Taifa Stars, Maximo alikuwa analipwa
dola 10,000 (zaidi ya Sh milioni 16) na alipongia mkataba wa mwisho
akaanza kulipwa dola 15,000 (zaidi ya Sh milioni 24).
Yanga ambayo
inaendelea kusajili kikosi imara chini ya usimamizi wa Yusuf Manji
unaoongozwa na kamanda wa jeshi lake, Seif Mohammed ‘Magari na Ahmed Bin
Kleb, imeamua kupata kocha wa uhakika ingawa kuna maombi zaidi ya
makocha 20 ambao wameomba kuinoa.
Kablaya kuondoka Maximo alimteua
Yondan katika kikosi cha Stars na kumchezesha pamoja na Nadir
Haroub
‘Cannavaro’, pia alisema Yondani ameiva kuichezea Stars.
Wakati
anajiandaa kuiachia Taifa Stars, Maximo alikuwa anawindwa na klabu
mbili, Orlando Pirates ya Afrika Kusini na nyingine kutoka nchini Israel
lakini mwisho aliamua kurejea kwao Brazil na kuendelea na kazi ya
kufundisha.
0 comments:
Post a Comment