MSANII kutoka nchini Burundi, Jean Pierre ‘Kidumu’, sambamba na
msanii wa muziki wa kizazi kipya, Peter Msechu, wanatarajiwa kupamba
shindano la kumsaka mrembo wa vyuo vikuu ‘Redd’s Miss Vyuo Vikuu Arusha’
litakalofanyika leo.
Akizungumza na waandishi wa habari, mwandaaji wa shindano hilo, Gaudencia Magessa wa Fame City Décor, alisema kuwa wasanii hao wanatarajiwa kutumbuiza katika usiku huo wa kumsaka mrembo wa vyuo vikuu mkoa wa Arusha; shindano litakalofanyika ukumbi wa Naura jijini hapa.
Alibainisha kuwa warembo 14 kutoka vyuo mbalimbali vya jijini hapa, ikiwemo Uhasibu Arusha, Makumira na vinginevyo watapanda jukwaani leo.
Alitaja zawadi kwa washindi kuwa ni sh 500,000 kwa mshindi wa kwanza, wa pili sh 300,000 huku wa tatu akiondoka na sh 200,000.
Alisema lengo la mashindano hayo ni kumpata mrembo wa mkoa wa Arusha, ambaye atakwenda kuwakilisha vyuo vikuu vya mkoani hapa, pia nia ya kusaidia jamii mbalimbali za mkoani hapa, ikiwa ni pamoja na kugawa misaada mbalimbali katika vituo vya kulea watoto yatima pamoja na wale wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Alitoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Arusha, kujitokeza kwa wingi katika shindano la leo, kwani ni la kwanza na limeboreshwa.
Alitaja baadhi ya wadhamini waliofanikisha shindano hilo kuwa ni Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji chao cha Redd’s Original, Real Metal Graft, Modern Supermarket, Perfect Supermarket , Sg Resort, Mwandago Investments, Clouds fm, Tipple A fm, Libeneke la kaskazini blog, Mount Meru Pure Drinking Water pamoja na Kasse Store.
Wakati huo huo, kituo cha kulelea watoto yatima cha Hope Orphans, kimetoa shukrani kwa waandaaji wa shindano hilo kwa kuwapa msaada wa vyakula.
Msaada huo ni pamoja na mchele, sabuni, unga wa ugali, mafuta ya kupikia pamoja na maji ya kunywa.
Akizungumza wakati akipokea msaada huo, Lucy Juma, alisema kuwa, wanashukuru kwa kupokea msaada huo kutoka kwa warembo wao, kwani utawasaidia katika kipindi hiki, huku akitoa wito kwa wananchi kuendelea kusaidia vituo hivyo.
CHANZO:http://www.freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=36568

0 comments:
Post a Comment