Nitatoa tamko la kina baadae kuhusu kilichotokea lakini kwa ufupi ubovu
wa bajeti hii ni matokeo ya udhaifu wa Rais Kikwete, yeye ndiye
aliyesaini Mpango wa Taifa wa miaka mitano kama Kiongozi Mkuu wa Nchi
tena kwa wino mwekundu kama Amiri Jeshi Mkuu. Na yeye ndiye Mwenyekiti
wa baraza la mawaziri, bajeti hii iliyoacha kuzingatia mpango
wa Taifa imepita kwenye baraza alilloliongoza, pia kushindwa
kutekelezwa kwa bajeti iliyopita ni matokeo pia ya udhaifu wa taasisi ya
Urais.
Pia kwa mujibu wa Katiba Rais ndiye ambaye anapeleka
bajeti bungeni, Waziri mwenye dhamana anapeleka tu kwa niaba. Rais
amepewa mamlaka makubwa juu ya bajeti ibara ya 99 imeweka mipaka kuhusu
mambo ambayo bunge lina mamlaka nayo huku ibara ya 90 inasema bunge
likikataa bajeti rais ana mamlaka ya kuvunja bunge. Hivyo Rais Kikwete
anapaswa kuagiza Waziri wa Fedha bajeti iondolewe irudi kwenye baraza la
mawaziri ikafanyiwe marekebisho!
John Mnyika
19 Juni 2012
0 comments:
Post a Comment