Na Mwandishi Wetu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete,
anatarajiwa kuwa refa wa mchezo wa soka kati ya wabunge mashabiki wa
Simba dhidi ya Yanga.
Mechi ya wabunge hao mashabiki wa Simba na
Yanga, inatarajiwa kufanyika Julai 7, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam, ikiwa ni moja ya matukio yatakayopamba Tamasha la Usiku wa
Tumaini.
Meneja Mkuu wa Global Publishers, wanaoandaa tamasha hilo, Abdallah Mrisho, alisema kuwa wameshamuandikia barua JK ya kumuomba awe mgeni rasmi, vilevile awe refa wa mechi hiyo ya wabunge na kwamba matarajio ni mazuri.
“Tuna matarajio ambayo ni chanya kuhusu Mheshimiwa Rais kuingia uwanjani na kuchezesha mechi ya wabunge na kwa kweli hili litakuwa tukio la kihistoria kuwahi kutokea,” alisema Mrisho na kuongeza:
“

Tunaamini kwamba kitendo Mheshimiwa Rais kuchezesha
mechi hiyo ya wabunge, siyo tu kwamba kitawafurahisha wananchi
watakaohudhuria tamasha hilo la Usiku wa Tumaini, bali pia kitakuwa
faraja kubwa kwa kila mhudhuriaji na Watanzania kwa jumla.”
Katika
tamasha hilo, mbali na mechi ya wabunge, kutakuwa na mchezo wa soka kati
ya wasanii wa filamu Tanzania (Bongo Movie) dhidi ya wenzao wa muziki
(Bongo Fleva). Vilevile wanafunzi wa Shule ya Sekondari Makongo,
watachuana na wenzao wa Shule ya Sekondari Jitegemee.
Upande wa masumbwi, bondia Francis Cheka atamaliza ubishi na Japhet Kaseba, ikikumbukwa kwamba mara ya mwisho walipopigana, pambano lao halikufika mwisho.
Upande wa masumbwi, bondia Francis Cheka atamaliza ubishi na Japhet Kaseba, ikikumbukwa kwamba mara ya mwisho walipopigana, pambano lao halikufika mwisho.
Kuhusu burudani, wanamuziki wakali jukwaani, Joseph Mayanja
‘Chameleone’ na Nasibu Abdu Juma ‘Diamond’ watapambana kuoneshani ni
nani anatisha kwa kumiliki ‘steji’ ukanda wa Afrika Mashariki.
Wakali wa Hip Hop, Ibrahim Mussa ‘Roma’, Rashid Makwilo ‘Chidi Benz’, Kundi la Pah One na wengine wengi watakuwepo.
Wakali wa Hip Hop, Ibrahim Mussa ‘Roma’, Rashid Makwilo ‘Chidi Benz’, Kundi la Pah One na wengine wengi watakuwepo.
0 comments:
Post a Comment