Shimo ambalo mwili wa kichanga ulipatikana.
MTOTO
mchanga aliyezaliwa muda mfupi na kutupwa chooni katika eneo la Hosteli
ya Lilian Ngoyi katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) cha
Morogoro, anadaiwa kufanyiwa hivyo na mwanafunzi wa kike anayesoma hapo.
Tukio
hilo la kuhuzunisha, lilitokea Ijumaa iliyopita majira ya saa nne
asubuhi kwenye chemba (mifereji ya maji machafu) za hosteli hiyo ambazo
zilikuwa zimekwama kwa kufurika maji baada ya kichanga hicho kushindwa
kupenya kwenye shimo la chemba mojawapo.
Mmoja
wa wahudumu wa usafi chuoni hapo, Andrew Seluhimbo, ndiye aliyegundua
tukio hilo la kuhuzunisha baada ya kugundua kwamba kilichokuwa
kimesababisha kuziba kwa mifereji hiyo ni mwili wa mtoto mfu wa kiume.
Hii
ni mara ya tatu kwa miili ya vichanga kutupwa katika Manispaa ya
Morogoro katika kipindi cha siku nne ambapo mwanzoni ilitokea katika Mto
Morogoro eneo la Mji Mpya, ikafuatia huko Kihonda Mizani kabla ya hili
la eneo la SUA.
|
0 comments:
Post a Comment