Mabingwa wa mpira wa Miguu Tanzania Simba ya Dar es salaam, usiku wa
tarehe 13 May 2012 imeyaaga mashindano ya Kombe la Shirikisho barani
Afrika baada ya kufungwa magoli 3 - 0 na Al-Ahly Shandy ya Sudan kwenye
muda wa kawaida.
Magoli yote hayo yalifungwa katika kipindi cha pili, la kwanza likiwa
dakika ya kwanza kipindi cha pili, yakifuatiwa na jingine dakika 3
baadaye. La tatu lilifungwa baada ya dakika 10 baada ya goli la pili kwa
uzembe wa Victor Costa kwa kutokuwa makini na utoaji wa pasi na hivyo
kupoteza mpira huo uliomfikia mchezaji wa Al-Ahly Shandy aliyefunga kwa
urahisi. Mwisho wa dakika 90 mabao yalikuwa 3 - 0 dhidi ya Simba, na
hivyo kufanya kuwe na jumla ya mabao 3 - 3.
Mshindi alipatikana kwa njia ya penati ambapo jumla ya penati 10
zilipigwa. Juma Kaseja alishindwa kufunga penati ya mwisho kwa Simba na
hivyo kuzidiwa bao moja na Al-Ahly Shandy
Simba wanatarajiwa kurudi Dar es Salaam Jumatatu, ili waanze kuganga mashindano mengine.
Home
»
»Unlabelled
» Simba yatolewa Na Al Ahly Shandy kwa Penati 9 - 8
Monday, May 14, 2012
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment