Kampuni moja ya marekani SpaceX
imezindua roketi ya kwanza ya kibiashara itakayotumika kupeleka huduma
na bidhaa kwa kituo cha kimataifa cha angani.
Roketi hiyo inayofahamika kama Falcon-nine
iliondoka katika eneo la Cape Canavera jijini Florida baada ya jaribio
la kwanza kugonga mwamba siku ya jumamosi.
Inatarajiwa kuchukua siku mbili kufika katika kituo cha angani.
Ndege za serikali ndizo zimekuwa zikitumiwa
kusafirisha chakula na huduma katika kituo hicho lakini shirika la NASA
linataka kutoa huduma hiyo kwa kampuni za marekani za kibinafsi.
Mwandishi wa BBC ameeleza kuwa serikali inatumai
hatua hiyo itapunguza matumizi yake kwa mradi huo na badala yake pesa
hizo kutumika kwa utafiti zaidi katika anga.
0 comments:
Post a Comment